KISA CHA ANIA NA ALEX; AIBU YA UKWENI - EDUSPORTSTZ

Latest

KISA CHA ANIA NA ALEX; AIBU YA UKWENI

Teenage Boy Disappointed With Exam Results Stock Photo - 43051831
Ilikua ni mara yake ya kwanza kwenda kutambulishwa ukweni, walikua wamekaa mezani na wakwe zake wakila chakula ambacho kilikua kimeandaliwa na Mama mkwe wake mtarajiwa. Akiwa hana hili wala lile, Ania alianza kujisikia vibaya, bila kujijua alijikuta amejamba kwa sauti katikati ya chakula mbele ya wakwe zake.
Harufu ilianza kusikika na huku kila mmoja akimuangalia mwenzake kwa aibu Alex, mchumba wake alinyanyuka huku ameshika tumbo akainama akilalamika “Samahani sijui hata jana nimekula nini yaani tangu asubuhi tumbo linanisumbua… Mhhhhh!” Aliendelea kulalamika.
Alinyanyuka na kwenda kukaa kwanye kochi, Ania alimfuata, akimshika kama akitaka kumsaidia kutembea. Walipofika na kukaa Annia alimuangalia Alex na kumuambia “Ahsante mpenzi wangu…” Alex alitabasamu na kumuambia “Usijali niko kwaajili yako uko sawa mpenzi?
“Hapana, niondoe hapa nitaaibika, sijisikii vizuri kabisa…” Anie alimuambia Alex ambaye alinyanyuka kwa shida kidogo, alienda na kuwaambia wazazi wake hajisikii vizuri inabidi kupitia zahanati, alimpa Ania ufunguo wa gari ili aendeshe yeye kwani alidai asingeweza kutokana na hali yake. Waliondoka ndugu wakiamini kuwa yeye ndiyo alifanya tukio lile alibeba aibu ya mpenzi wake.
NB; Nikazi yako kwa wewe mwanaume/mwanamke kubeba aibu za mwenza wako kwa ndugu zako kwani ndugu zako hawawezi kukuchukia lakini wanaweza kumchukia mwenza wako!
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz