1. Kama upo SINGLE na umekazana kusema "SIAMINI MTU KATIKA MAPENZI" kumbuka rafiki zako wanaoa na kuolewa kila siku. Acha mawazo hasi omba Mungu akujalie mwenza wa maisha ambae unaendana nae.
2. Kama upo ndani ya ndoa na umekazana kusema "NAICHUKIA HII NDOA" huoni wanandoa wengine ambao wanasheherekea jubilei ya miaka 20 ya ndoa zao? Omba Mungu aiponye ndoa yako.
3. Kama umekazana kusema "NAMWACHA MUME WANGU, KWANI ANANISALITI" tafadhali hebu nenda mjini pita maeneo ya Kona Bar, Kimboka na maeneo kama hayo uone wanawake malaya wenye uchu ambao wanamsubiri kwa hamu mumeo wamchune vizuri ambao kwao hawajali haya ku share mwanaume. Omba Mungu aitengeneze ndoa yako.
4. Usikazane kusema "NAICHUKIA KAZI YANGU" angalia maelfu ya vijana ambao hawana ajira wanazunguka kila siku na mabahasha maofisini! Vipi unataka kujiunga nao? Kuwa na shukrani!
5. Umekazana kusema unapachukia unapoishi, tafadhali sana nenda kawatembelee watoto wa mitaani uone mazingira magumu wanayoishi! Mshukuru Mungu walau unalala hata kwenye godoro.
6. Wengine husema "NIMECHOKA NA HAYA MAISHA" sawa nenda mahospitalini na uone watu wanavyopigania maisha yao, nenda mochwari na utizame na uniambie unafikiri nini! Cha Mihimu ni kushukuru Mungu
Hebu nisikilize kwa makini......
Kutambua thamani ya miaka minne au mitatu, muulize mhitimu wa chuo kikuu
Kutambua thamani ya mwaka mmoja, muulize mwanafunzi aliyefeli mtihani wake wa mwisho, kutambua umuhimu wa miezi tisa muulize mama aliejifungua mtoto aliye njiti!
Kutambua thamani ya wiki moja muulize mhariri wa gazeti linalotoka kila wiki.
Kutambua thamani ya dakika moja muulize abiria aliyechelewa safari ya ndege, basi au treni.
Na kutambua thamani ya sekunde muulize mtu yeyote aliyenusurika katika ajali!
Furahia kila dakika ambayo mwenyezi Mungu amekupa kuendelea kuvuta pumzi yake! Acha kulalamika maisha ni jinsi wewe unavyoishi!
Kama upo hai mpaka leo shukuru kwa kusema "ASANTE MUNGU"
Share uwezavyo!
Post a Comment