HAYA NDIO MAMBO 10 AMBAYO YATAMFANYA MKEO KUWA NA FURAHA SIKU ZOTE NA KUJIVUNIA KUWA NAWE. - EDUSPORTSTZ

Latest

HAYA NDIO MAMBO 10 AMBAYO YATAMFANYA MKEO KUWA NA FURAHA SIKU ZOTE NA KUJIVUNIA KUWA NAWE.

Irene Uwoya - Fashion on point !!! @serena_karis . >... | Facebook
1.Wahi kurudi kwa mkeo ili ata watoto wakuone, yeye sio mlinzi wa nyumba yako
2.Msaidie ata kusomba maji, kufagia uwanja kupika na ikibidi kukosha vyombo ili asijute kuolewa nawewe. Usimfanye housegirl au punda wako tambua thamani yake yeye ndio mama watoto wako na zaidi mke wa maisha yako.
3.Mfanye mkeo awe na furaha wakati wote, asiwe kama mpira na kumtolea maneno machafu na masimango.
4.Kipindi unaanza nae ulimpa sifa kedekede kwamba "You are the special one hny" basi endelea kuonyesha sifa ulizompa aringe kwa wenzie wanaokaa vibarazani
5.Usipende kumfananisha mkeo na wanawake uliopita nao huko kwasababu wewe ukiugua yeye ndo hupata shida ya kukuuguza na nakulea watoto.
6.Hajachuja, tatizo matunzo humpi sasa atang'ara vipi? Huyo wa nje anaekuona handsome ni kwasababu wa ndani anakujali nakukupa heshima na sifa zote kama mume.
7.Acha kua mkali kwa mkeo mpaka watoto wakikuona wanaona kama simba kaingia wanakimbia kujificha.
8.Muheshimu mkeo kwakua hakuna aliyekuchagulia, ulimpenda mwenyewe ukaita watu waje washuhudie na vigelegele wakapiga.
9.Mpende nayeye atakupenda maana kichwa cha nyumba ni kiongozi bora kwa familia (mkeo na watoto)
10.Samahani kwa mkeo ni neno kubwa sana hata kosa liwe kubwa kiasi gani atakusamehe tu, ila ogopa sana mwanamke akishasema bhasiiiiiiii...........
JAMANI NDOA SIO MCHEZO WAKUIGIZA, MPENDE MKEO, HAJUI MFUNDISHE ACHANA NA HUYO WA PEMBENI HAWEZI KUKUPA FURAHA KAMA MKEO WA NDOA
NB: Maneno yangu sio sharia
KAMA umenielewa SHARE na marafiki zako post hii
Nakutakia siku Njema, Mungu Akubariki na kukulinda
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz