🌸BARUA YA 07: WAJIBU WA MKE MWEMA KWA MUME WAKE🌸 - EDUSPORTSTZ

Latest

🌸BARUA YA 07: WAJIBU WA MKE MWEMA KWA MUME WAKE🌸


Ndugu zangu wanawake napenda tushirikishane mambo machache ambayo ni muhimu kuyatenda kwa mume wako.
Mke anatakiwa kufanya mambo yafuatayo ambayo ni tunu za upendo wake kwa mume wake.
1. Mke unatakiwa kuwa msikivu na mtii kwa mume wako,
2. Mke unatakiwa kumshirikisha mumeo mambo mbalimbali yanayokuhusu.
3. Mke unatakiwa kujua hisia za mume wako na kumsoma,
4. Mke unatakiwa kuwa mnyenyekevu kwa mumeo.
5. Mke unatakiwa kutambua changamoto za mume wako katika shughuli zake za kila siku.
6. Mke unatakiwa kujua namna ya kuzungumza na mumeo na hasa wakati unaofaa.
7. Mke unatakiwa kujua kuwa mumeo ana sehemu ya ubongo wake ambayo inaitwa “nothing room” anakuwa katika kipindi hichi mpe nafasi mumeo.
8. Mke lazima utambua kuwa ubongo wa mumeo na wa kwako unatofautiana, “wanawake wa multi-task brain na wanaume wana mono-task brain” hivyo unavyomweleza mumeo jambo fulani mpe muda ya kuritafakari, siyo unamwambia mambo mengi kwa wakati mmoja, ndiyo maana wanaume wengine atakuangalia tuu na kuondoka bila kukujibu.
9. Mke unatakiwa kutambua kuwa mumeo pia ni kama “mtoto wa mkubwa wa kiume”.
10. Mke ni wajibu wa kutambua kuwa maisha ya ndoa, ni maisha ya kusaidiana, Msaidiane na kushauriana na mumeo.
© Theddyna Ministry.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz