ZIJUE DALILI KUMI ZA MWANZO KABISA ZA UJAUZITO…. - EDUSPORTSTZ

Latest

ZIJUE DALILI KUMI ZA MWANZO KABISA ZA UJAUZITO….

No photo description available.



Ujauzito ni nini? Hii ni hali ya mwanamke kubeba kiumbe kwenye mfuko wake wa uzazi, dalili za ujauzito wakati mwingine huweza kuchanganya watu na magonjwa mengine kama malaria na magonjwa ya njia za mkojo hasa mwanzoni mwa ujauzito, lakini pia kuna watu hawazipati dalili hizi na kushtuka mimba ikishakua kubwa kabisa.
Mimi kwa uzoefu wangu nimeshakutana na wanawake watatu katika vipindi tofauti wakiwa na ujazito wa miezi sita bila wao kujua wakihisi ni unene tu..
Dalili za ujauzito husababishwa na kuongezeka kwa kwa hormone za uzazi ndani ya mfumo wa damu wa mwanamke..lakini kabla ya kwenda kuhakikisha ujauzito na vipimo vitu vifuatavyo huonekana kwanza kwa mwanamke husika..
· Kukojoa mara kwa mara
· Kutoona siku zako
· Kichefuchefu na kutapika
· Matiti kuuma na kuvimba
· Kuchoka sana bila kazi
· Kupoteza hamu ya kula
· Kupata hasira au furaha ndani yam da mfupi.{mood swings}
· Kizunguzungu
· Kuongezeka joto la mwili.
· Kuongezeka kwa uwezo wa kunusa harufu.
Ukiona dalili hizi kimbia ukahakikishe na vipimo kwani inweza kua tayari umepandikizwa kiumbe ndani ya mfuko wa uzazi.




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz