Usisahau kumwambia mke wako ❤️ NAKUPENDA❤️ kila siku, ili imsaidie kumpa faraja na matumaini.
Vilevile, usisahau kusema neno 🙏 ASANTE🙏 kila baada ya kushiriki tendo la ndoa, ili kuonyesha kuwa umethamini huduma uliyopeewa.
Vilevile , akimaliza kukupigia nguo pasi, kukufulia, au kukuwekea maji ya kuoga bafuni, kumbuka kumwambia ASANTE MKE wangu”
Ifanye ndoa yako kuwa paradiso kwa kuepuka namna zozote zinazoweza kuleta machafuko ndani ya ndoa.
Aidha ukumbuke kuwa ,maudhi ya kila wakati ni tatizo, na yanaathiri amani ya ndoa. Kwahiyo, wanandoa wanashauriwa wawe makini katika hili, ili amani ya kweli itawale katika nyumba yenu siku zote.
Ukipata nafasi siku ambazo upo nyumbani, msaidie mke wako shughuli ndogondogo za hapo nyumbani, mathalani; kupika, kufua nguo au kufagia mazingira ya hapo mahali mnapopishi, kama sehemu ya kuonyeshana upendo na mapenzi baina yako wewe na mke wako.
Usikubali ndugu zako, wamnyanyase mke wako badala yake uwe imara na umlinde mkeo.
No comments:
Post a Comment