UNAPENDWA PENDEKA.....ACHA KULINGA UTAKUJA UJUTE BAHATI HAIJI MARA MBILI. - EDUSPORTSTZ

Latest

UNAPENDWA PENDEKA.....ACHA KULINGA UTAKUJA UJUTE BAHATI HAIJI MARA MBILI.

Image result for MAISHA YA UPENDO YA MUME & MKE YANAJIONYESHA KWA MAMBO YAFUATAYO

Hakuna kitu kigumu kama kupendwa wengi wapo kwa ajili ya vitu na wala siyo kuhitaji kufanya maisha na wewe kuunda familia yenye upendo na kufikilia kusonga mbele kimaendeleo.
Wengi mmekua mkiwapoteza watu sahihi kwenu kwa kushindwa kuiona dhamana ya upendo na mapenzi ya dhati mlivyokabidhiwa ndani ya mioyo yao.
Badala yake mmeitumia nafasi ile kuwatesa na kuwanyanyasa kiroho kisa mmejua ukweli kwamba mnapendwa na hakuna zaidi ya wewe ndani ya moyo wake.
Sasa imekua njia ya kujivunufaisha tu kila wakati kujinunisha tu kila wakati kuomba vitu vya gharama na kuwapelekesha wenzenu kwa kujua lazima atatimiza kisa anakupenda na hataki kukupoteza.
Umesahau kua mwenye mapenzi ya dhati ni kawaida kabisa na inampasa akupende ili ufurahie kupendwa huko na ujiongeze kua huna haja ya kuhangaika na manyau mengine ambayo yangekudangaya na kukuumiza lakini wewe umeichukulia like a point of weakness kumusumbua mtoto wa watu kumuchuna na kumuendesha kana kwamba hana moyo wala hauminii.
Unataka upendweje ili ujue kwamba huyo ni mtu sahihi kwako.. Ubebwe mgongoni utembezwe toka masaki mpaka ukonga au unataka akuogeshe kwa kukulamba mwili mzima?
Kwa nini hupendeki.. Ona ulivyo mpoteza huyo wa kwanza kwa kujikuta tu huelewi kua unapendwa na yupo tayari kufanya maisha na wewe..
Sasa hivi napo Mungu amekupa mwingine ni yale yale umeanza hivi unadhani uzuri wako huo utadumu milele bila kua na mmoja wa kukutunza na kukupa amani...
Hivi unadhani shilingi zako hizo utakua nazo siku zote mpaka uhisi ndio zinapelekewa upendwe?
Hivi uoni kinyaa cha kubadilisha midomo ya denda kama mirija ya juice thamani yako iko wapi kama hujaamua kubaki ja mmoja anayekupenda mpaka na wewe unajua..
Usiichezee nafsi hiyo ambayo leo imekupa dhamana ya kukupenda na upo peke yako moyoni mwake
Fikiria mapungufu yake yanarekebishika na yanaisha tu kwa sababu anakupenda yupo tayari kukusikiliza na kufuata unachotaka
Ridhika na ipokee furaha ya mwenzako ya kua na wewe.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz