ππUnaweza kuwa fundi wa kukata mauno kitandani, bafuni mpaka jikoni na kuchana misamba kwa kiwango kikubwa lakini bado ndoa ikakushinda.
ππUnaweza kumpa mwanaume kila atakacho lakini bado akachepuka hata kukufanya kujiuliza hiyo michepuko imekuzidi nini?!!?! Maana kama kufundwa umefundwa ukafundika juu ya kumtunza mume na kumpa haki yake ya ndoa.
ππWengine wamefikia hatua ya kudhani labda wanazidiwa ufundi kwa kuwa michepuko inatoa tendo la ndoa kinyume na maumbile ama wanatumia dawa za kienyeji kutoka kwa waganga wa kienyeji.Mbaya zaidi wengine wamejikuta nao wakitamani kuwapa waume zao kinyume na maumbile ama kwenda kwa waganga wa kienyeji wakidhani labda ndiyo itakuwa suluhisho la ndoa zao.
ππNataka kukuambia suluhisho la ndoa ni uchaMungu,
ππKuwa mtu wa ibada kwa wingi na muombee mumeo au mkeo, watoto na familia kwa ujumla ili kuwe na amani na upendo wa kweli.
No comments:
Post a Comment