Sometimes wanawake huwa wanajiuliza maswali mengi, wafanyeje ili wapendwe, wanahisi wana bahati mbaya. - EDUSPORTSTZ

Latest

Sometimes wanawake huwa wanajiuliza maswali mengi, wafanyeje ili wapendwe, wanahisi wana bahati mbaya.


Kila wanapoitoa mioyo yao mabwana wanakula mzigo wanatembea.
Mioyo yao imejaa matundu hawaamini kabisa kama wanaume huwa wanapenda.
Imefikia wakati wanadhati wanaume hutamani tu, kumbe sio kweli.
Wanaume tunatest zetu hatuendi tu kama mbwa koko, jalala moja baada ya jingine, HAPANA.
Sifa za mwanamke ambazo mwanaume atavutiwa na kukaa nae ni hizi zifuatazo:
JITAZAME KAMA HUNA ANY OF THESE ni heri ujifunze kuwa nazo.
 BADO HUJACHELEWA.
(1)MWANAMKE MWENYE MSIMAMO.
Jambo moja muhimu ambalo mwanaume anaangalia kwa mwanamke ni msimamo wako:
Sio mwanamke upo kama feni, kila sehemu unapuliza upepo; mashariki, mgharibi, kaskazini na kusini kote wewe. Hapo sahau tena sahau sana.
Mwanaume anahitaji kuwa na uhakika kwamba mwanamke alie mkabidhi moyo wake hana mishe mishe na hayumbishwi na lolote, na chochote na penzi lake lipo safe.
Unaweza kuwa na kila kitu, mzuri wa sura, umbile na kila kitu na usimpate mwanaume wa maana kama huna sifa hii;
Hakuna muujiza kwenye hili, ndo wanaume tulivyoumbwa; kama huko hivyo hutopata mwanaume wa maana, utapata vimeo kama wewe ulivyo.
(2)MWANAMKE MUELEWA
Men are simple creatures, they love to live simple; take them simple as they are.
Ukiwa aina ya mwanamke una’mind vitu,.. kitu kidogo tu ugomvi, unaongea na nan, uko wapi, na nani, unafanya nini huko, kwanini, heee jamani kama mahakama kuu?
Hapa utapoteza credit; kuwa aina ya mwanamke muelewa ambae utamfanya mwanaume ajisikie vibaya kufanya kitu flani ambacho ulisha mwambia asifanye before.
Sio kukaripia na kununa, let him realize that amefanya kitu cha kukuudhi na huja’react, kama mwanaume alie kamilika atajua amekosea na ataomba msamaha:
Ila kama janaume gume gume ndo basi tena litakausha na ndo inakuwa issue.
Jua lugha ya kutumia ambayo utafikisha ujumbe and yet you don’t show him kama ume’mind, usimkaripie.
Kumkaripia mwanaume ni msala mpya, hata kama anakosa ataku’mind na itakula kwako.
(3)MWANAMKE DIRECTOR
Baba ni kichwa cha nyumba/familia; mama ni macho yaliyo kwenye kichwa hicho, women play a very vital role in DIRECTING THE HEAD TO THE RIGHT WAY: kichwa bila macho si utajigonga tu?
Mwanamke ni jicho: ukikalia kujiremba tu na kuwaza mambo mengine bila kujua kuna kichwa kinasubiri maelekezo yako utaonekana bogasi.
Kutwa kwenye umbea huna muda wa kujua ur man anaplan gani mwaka huu, unamsaidiaje kuzifikia, sasa we faida yako nini kwenye maisha yake?
Be a kind of a woman ambae mwanume aki-achieve jambo anasema i have a woman on my side who Engeneered this.
Kama hujawahi kufikia hatua ya kuwa appreacieted kwa ur man kwa jambo hili bac jua kuna mahali umefeli.
Na hili haliji hivi hivi, linakuja pale panapokuwa na proper communication between u & ur man.
Bila good communicatio.
(1)Hutojua what ur man is up to.
(2)Kwakuwa hujui what ur man is up to, hutokuwa na msaada.
(3)Akifaulu jua haupo kwenye picha ya mafanikio yake and ur simply useless.
(4)Akifeli; u are a part of his failure kwamba humsaidii lolote; u are simply useless,
U HEAR ME?
Sababu uwepo wako haumsaidii. Women have plan and control ability; USE IT: U HEAR ME?
Usikae tu kama muuza genge unasubiri wateja, DO UR JOB and win him.
(4)MWANAMKE MSAFI:
Usafi huu sio wa nguo tu na kunukia, ni zaidi ya hivyo, usafi unaanzia ndani, msaidie mwanaume awe msafi pia, rohoni hadi mwili.
Jitu haliswali, halikumbuki kama kuna M/Mungu, lipo tu; unadhani mtajenga familia gani baadae?
Msaidie kum’remind kumkumbuka muumba, mafanikio ya nje huanzia ndani, mambo mengine anafanya nje na yana’affect kwa sababu umefeli ku’inspire change ya ndani.
Kama patakuwa na usafi wa ndani everything outside will be set automatically.
Sio kazi yako unamkumbusha baby hatuendi CLUB oo lets go out; unamkumbusha KUSWALI?
Utakuja tengeneza mwanaume freemason bila kujua, we haya.
Huu usafi mwingine wanawake mmejaaliwa mashaallah, miili yenu misafi kiasi biashara ya kunuka kikwapa no; kusafisha nyumba mnasafisha vyema, saaaafi.
Unaweza ukamfanya man wako aone potential hata kama wewe sio mzuri sana, lakini anaona kiongozi wa familia inside you, and he will definitely apt you.
Hamna limbwata wala nini, tupa kule.
Kama huna hizi SIFA nne 4 aisee waza upya; unaweza bahatisha ukaolewa lakini usitegemee muujiza, goma litapata pacha tu:
Jamaa atajutia mahari aliyolipa, atasepa kimya kimya
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz