SALAAMU ZANGU ZA VALENTINE KWA MABINTI. - EDUSPORTSTZ

Latest

SALAAMU ZANGU ZA VALENTINE KWA MABINTI.


Mabinti zangu,wadogo zangu na dada zangu yumkini nisipate muda wa kuongea na ninyi kesho au nikaja kusema nikiwa tayari nimeshachelewa.
Naomba niongee yumkini maandishi haya yakaponya hatma ya mtu mmoja.
Kesho ni tarehe inayoitwa Valentine,ambayo wengi wameiita siku ya wapendanao.
Well;ni siku ya kuonyesha upendo kwa yule umpendaye aweza kuwa mzazi,mpenzi au hata rafiki.Siku hii sio siku ya watenda dhambi /kutenda dhambi kama ambavyo wengi walivyoitafsiri na kuichukulia.
Hatma /future za wengi zimeharibika kwasababu ya siku hii,kuna watu mpaka sasa hawataki kabisaa kusikia hii tarehe maana ndio siku ya wao waliyoambukizwa virusi vya ukimwi, na sasa wanaishi kwa majuto.
Kuna watu siku hii ndio walijikuta wamebeba ujauzito pasipo kutarajia,kuna watu siku hii ndio walijikuta wamesimamishwa na kufukuzwa masomo,kuna watu tarehe hii ndoa zao zilivunjika,kuna watu tarehe kama hii ndio tarehe walifukuzwa makwao na wakaenda kuharibikiwa kabisaa.
MY TAKE.
Kama huna sababu kuu ya msingi ya kesho kukufanya utoke nyumbani na kwenda kukutana na mtu tafadhali nakushauri kaa zako nyumbani.
Kama ni zawadi unaweza kujinunulia,kama ni outing una hela yako jitoe usikae ndani ,kama ni Neno I LOVE YOU unataka kusikia jiambie mwenyewe. Lakini chonde chonde usiende kuharibu hatma yako kwasababu ya vitu hivyo hapo juu.
Hata siku ikipita kimyaa mshukuru Mungu iko siku utakuwa naye wa halali au wewe mwenyewe ukajipenda.
Dont allow a single one act of one day destroy your whole future.
Dont trade yourself for the sake of Valentine Day,your value is beyond that word and day and date,you are virtuous and honoured vessel of God.
Kama kuna miadi ya kesho na mtu ambaye ukiwaza unaona kabisa lazima ukaanguke dhambini nakushauri cancel haraka miadi /appointment hiyo waza zaidi juu ya hatma yako na sio chips au burger,pizza na soda.
HAPPY VALENTINE IN ADVANCE
Pastor Winnie Kilemo




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz