PESA NA SE=X ZINAVYOHARIBU MAHUSIANO - EDUSPORTSTZ

Latest

PESA NA SE=X ZINAVYOHARIBU MAHUSIANO


Image result for UNATAKA KUJUA NI KWANINI WANAUME NDIYO HUONGOZA KWA KUTELEKEZA WATOTO WAO?
-Katika kizazi cha leo, ukiondoa Se=x katika mahusiano utagundua kuwa asilimia kubwa ya wanaume hawana jambo lingine la maana la kuwepo katika mahusiano. Vilevile ukiondoa pesa utagundua asilimia kubwa ya wanawake hawana jingine wanalohitaji katika mahusiano.
-Bila pesa Asilimia kubwa ya wanawake wengi wataona haina haja ya kuwa katika mahusiano. Na bila Se=x, utagundua kua wanaume wengi hawaoni haja ya mahusiano. Huo ndio ukweli ukatae, upinge, ulie ila sio wote wengine hawana mambo haya kama mimi na fulani .
-Namnukuu dada mmoja hivi, alisema
"Sisi wanawake tunataka Boyfriend wetu watutunze, lakini hakuna cha thamani tunachokiongeza katika maisha yao zaidi ya kuwapa se=x tu"
-Wanawake nao wanalalamika kwamba wanaume wanapenda sana se=x basi wakishapata se=x wanawakimbia na ule upendo waliokua wakiuonesha mwanzo unapotea.
-Ni wakati wetu sote kubadili mtazamo Mwanamke na mwanaume badili fikra zako sasa. Kaka mahusiano sio se=x tu dada angu mahusiano sio pesa tu. Mahusiano ni zaidi ya pesa na s=ex, Wanaume wengi siku hizi wanalalamika sana kwamba wanawake wanapenda pesa, sio wote ila baadhi yenu ni kweli mmeweka pesa kipaumbele. Na vile vile ni kweli asilimia kubwa ya wanaume wako after s=ex.
-Unakuta Mwanamke umeingia naye kwenye mahusiano anaanza baby nataka simu tena anasema na Aina ya simu cjui zile zinaitwa IPhone mara cjui zile Kama tunda Apple cjui, baby nina shinda na laki tano naomba baby wangu.
-Mara bby nataka hiki na hiki Mara baby rfk yangu (---) ana birthday nataka kumununulia zawadi ya saa na keki Mara cjui nataka hiki na hiki daaaah mwanamke anapenda pesa kama Saccos ya wachaga looooh
-Pia kuna wanaume wengine wanachekesha Sana inakomaa na mwanamke siku za mwanzo ila akishapata penzi tu utashangaa huyoo anamute Kama ameibiwa simu, mawasiliano yanapungua mapenzi ndio yanaanza kufifia hili ni tatizo kubwa Sana unakuta mwanaume ana wanawake wengi kama salone ya dada Bhoke.
-Ila mwanamke mpya atamjali, atamcare, atakuwa ladhi kufanya lolote ili amfurahishe tu ila dada angu akishakupata tu naye analala mbele Kama gari imekata Break
-Tujifunze kuongeza thamani katika mahusiano. mahusiano sio kupelekana kula bata na lodge za Mafichoni bali ni kuombeana tunapokuwa chini, kutiana moyo kuendelea kupambana na maisha.
-Kusaidiana hata kimawazo ya maisha, kusikilizana, na kupeana ushauri wenye tija, that's smart dating. Mkaka anakuambia baby Leo Sina pesa kbsa mama angu muelewe Kama mpenzi wako. Ila sijamaanisha wanaume musiwape wanawake wenu pesa la hasha kama ana shinda msaidie, mununulie zawadi umpe, ndio mahusiano yenye tija
-Inakua ni kazi bure pale ambapo mwanaume unajua jinsi ya kutengeneza pesa lakini unapata mwanamke ambae anajua kutumia tu. Ndio maana kwenye mahusiano ni vema nyote wawili mkawa na falsafa moja kuhusiana na pesa.
-Vinginevyo utakua unacheza Soccer safi la kushambulia, lakini defence ni dhaifu mno kama ya Singida United Itakua ni ngumu kwa hiyo timu kushinda unafunga matatu ww unafungwa saba haitajalisha ni kwa kiasi gani inao washambuliaji makini wanaozifumania nyavu. Na mwanamke ni kama safu ya ulinzi.
-Kaka angu na Dada angu pesa na s=ex sio kila kitu kwenye mahusiano kuna mambo mengi ya kufanya kwenye mahusiano zaidi ya hayo, mpende baby wako, mjali baby wako siku zote za maisha, usiwe na wanaume au wanawake wengi kwenye mahusiano utakuwa unaumiza akili yako bure kujibu watu ambao hawapo kwenye future yako ya maisha.
-Mchague mmoja baby wako namba moja muanze safari ya maisha pamoja mkiwa chini Kwenye ujana wenu hadi muwe mume na mke. Achana na vishawishi vya Pesa, achana na hulka za kufanya S=ex. Mpende bby wako namba moja hata hana pesa mtengeneze boy wako. ...
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz