MWANAMKE USISHINDANE NA MWANAUME KWA KUJIONA UNAWEZA⛔ - EDUSPORTSTZ

Latest

MWANAMKE USISHINDANE NA MWANAUME KWA KUJIONA UNAWEZA⛔


Image may contain: 2 people, people sitting
Wanawake wengi wamejikuta wanazama kwenye MAUMIVU MAKALI bila kujua chanzo, Nimebaini kwamba WANAWAKE wengi wamejikuta wanaolewa na wanaume ambao hawakuwatarajia ila ni kutokana na WALIOWATARAJIA KUTOONYESHA KWAMBA WATAKUWA WENZA WAO.
Pamoja na UVUMILIVU wa Mwanamke kusubiri pengine kungetokea mabadiliko lakini haikuwa pengine kwa wakati ama kwa sababu, Na Mwanamke kukata tamaa ya kuendelea hata akajinasibu kutafuta Mtu mwingine ambaye yeye Mwanamke ataweka sharti la NDOA na kwakuwa Mwanaume ni kama PANYA hachagui kichaka anajikuta AMEJITWALIA MKE bila kutarajia, Wakati huo huo Mwanamke anajikuta ameolewa na Mtu ambaye hakuwa ndiye chaguo lake, Mwisho kabisa wa NDOA HIYO NI MASIMANGO😭
Kila mmoja akitamba ki vyake lakini ambaye itamgharimu ni MWANAMKE kwa sababu unakuwa na aina mbili ya MAUMIVU;
 KUMKOSA ALIYEMPENDA.
 KUDUMU KATIKA NDOA NA MTU AMBAYE HAKUMPENDA.
Moto wake uwakao MOYONI ni dhahiri HUWEZI KUSALIMIKA
Shauku ya NDOA imewagharimu wengi, Kwamba Mtu aliweza kuwa kwenye MAHUSIANO miaka 3 alifurahia sana MAPENZI Lakini alipomkosa aliyempenda na kuolewa/kuoa Mtu mwingine wiki moja kwenye ndoa hiyo ni Sawa na MIAKA KUMI Yaani kila kunapokucha wazo kuu ni namna gani nitachomoka😅
Kusubiri kunawapasa wenye MIOYO YA UVUMILIVU na hao mara nyingi hushinda mitihani yote💪
Wanawake punguzeni kuyapenda MAGAUNI YA HARUSI👗 wala msipende chereko chereko za marafiki pamoja na ndugu, Hao wanabaki kuwa MASHUHUDA TU na wala hawataingia kwenye kukusaidia wakati wa MATESO YAKO KWENYE NDOA ambayo hukuitarajia, Balaa kubwa ni pale unapoanza kuishi na Mtu ambaye hukumtarajia kwa kifungo cha NDOA niamini pamoja na kutomtarajia lakini Kuna kitu kitakugharimu kuachana nae MAZOEA.
Mazoea yanajengwa na UKARIBU hata kama hamko kwenye GOOD TERMS lakini unaweza kujikuta HUTAMANI KUACHANA NAE wakati huo huo huhisi KUMPENDA 😅 na hapo ndipo utajikuta njia panda mara na ka mimba kamepenya weeee utabakia kuwa MHANGA wala usijue MBIVU ni zipi na MBICHI ni zipi? Uonapo uliyempenda Bado hajawa tayari kwa utakayo jipe muda kuendana nae ili usije jikuta UMEMUACHA kwa kujiamini kwamba utampata mwingine kwa MASHARTI yako niamini UTADUMU KWENYE UNYONGE.
#Elista_Kasema_ila_Sio_Sheria 🔨
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz