MUOGOPE SANA MPEMZI WA AINA HII

 Mtu anayeongelea Maungo yako tu kila story unajiuliza tu likitokea janga atakaa? Unaweza kuolewa na Chuchu mwiba kabisa, kashepu ka mchoro, katumbo flat kama Kim Kadarshian. Baada ya uzazi wa kwanza kitambi kikafumuka, nyonyo likawa kandambili za Joti, mwili ukajaa michirizi kama mgawanyiko wa nchi kwenye ramani ya Africa. Sasa Huyo jamaa ambaye amependa mwili tu na maungo atabaki na wewe?
Make sure mtu akupende wewe yani kuwe na kitu zaidi ya ngono kinachoweza kuwafanya kukaa pamoja na bado mkawa na furaha. Kuna reaction za Tembe za uzazi zinaweza kufanya uka-bleed Mwaka mzima, kama Huyo jamaa hakupendi wewe anapenda tu ngono na wewe lazima atachepuka.
Tafuta kitu zaidi ya gari na nyumba na hela za mwanaume ili upendo wenu udumu. Maana ukimpendea hela na wewe ukazipata hiyo Ndoa inakuwa haina jipya. Ndio maana nasisitiza muwe marafiki kwanza, mtafute namna ya kufurahiana bila ngono.#KIBONDE
Counsellor


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post