MPE MPENZI WAKO SABABU YA KUWA NA WEWE!!!SOMA HAPA KUJUA NAZUNGUMZIA NINI..... KARIBUNI - EDUSPORTSTZ

Latest

MPE MPENZI WAKO SABABU YA KUWA NA WEWE!!!SOMA HAPA KUJUA NAZUNGUMZIA NINI..... KARIBUNI

 kwenye uwanja wetu tujadiliane kuhusu mapenzi. Marafiki zangu, katika uhusiano umakini wa hali ya juu huhitajika ili uweze kuwa bora kila siku na kuufanya uhusiano wako kuwa wenye nguvu na usiotetereka! Katika hili hutegemea zaidi jinsi unavyoendesha uhusiano wako.
Ukitaka mpenzi wako akuchoke au umchoke, wewe ndiye mwamuzi, lakini pia ukitaka mpenzi asikuchoke au usimchoke wewe ndiye mwenye uamuzi kwa kuwa una uwezo wa kuyafanya yote hayo. Hebu nikuulize, umempa sababu mwenzako ya kuwa na wewe?
Je, unafanya nini kumfanya mwenzako asifikirie kabisa kuwa na mwingine zaidi yako? Kama nilivyotangulia kusema mara kadhaa huko nyuma kuwa, mapenzi ni sanaa marafiki zangu. Kuna wakati ubunifu unahitajika ili kumfanya mwenzako ajisikie fahari na faraja kuwa na wewe.
Wengi hawaelewi kuhusu hili, anaingia kwenye ndoa na mke wake au mumewe lakini baada ya muda anajikuta mapenzi yakipungua siku hadi siku mpaka anafikia hatua ya kuwa na mtu mwingine nje ya ndoa. Siyo sawa!
Inawezekana ukaendelea kuwa bora kwa mpenzi wako, inawezekana mpenzi wako akaendelea kuwa bora kwako ikiwa utahitaji kufanya hayo kwa dhati. Hakika kama ukitaka unaweza kuendelea kuwa wa kisasa katika uhusiano wako.
Yapo mambo ambayo ukiyafanya kwa ufanisi mkubwa, basi wewe utaendelea kuwa bora kwake naye atakuwa bora kwako. Hakuna kuchokana tena. Bila shaka sasa, hapo utakuwa mwenzi wako sababu hasa za kuwa na wewe. Hebu twende tukaone...
RUDI MWANZO KABISA
Siku zote nimekuwa nikisisitiza kuwa, jinsi unavyoanza ndivyo utakavyomaliza! Waswahili hawakuishia hapo, wakaongeza kuwa: “Unavuna kile ulichopanda!” Naamini katika semi hizo kuna mambo umejifunza.
Kama ulianza vibaya uhusiano wako tegemea kumaliza vibaya, lakini kama ulianza vizuri basi tarajia maisha mazuri ya kimapenzi yasiyo na maumivu katika moyo wako.
Kama unatarajia kuingia katika uhusiano na mpenzi mpya hakikisha hujionyeshi tofauti na hali yako halisi ilivyo. Jifunze kujikubali, hata kama unafanya kazi ambayo unadhani ni ya hadhi ya chini, mbainishe mpenzi wako hali halisi ilivyo.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz