Message kwa Dada wenye Tabia hizi 👇👇👇. - EDUSPORTSTZ

Latest

Message kwa Dada wenye Tabia hizi 👇👇👇.Image may contain: 1 person, standing, walking and outdoor

Wewe ni msichana mzuri, unapenda kwenda na wakati. Umeshaanza kutumia vilevi. Tena vile laini ambavyo ukinywa leo unaweza kulewa kesho.

Una mahusiano na John. Lakini unampenda sana Simon. Japo mvulana aliyekutoa bikira ni Side lakini toka muachane humuhitaji tena kwakua unamuona mshamba na unaona kabisa kua ulikosea njia kuwa nae.

Sponsor Molito ni baba unaye muheshimu sana. Kwakua uki date nae tu basi unarudi na pesa kibao

John hana pesa nyingi, ila bishoo. Ana rasta kichwan na kifua kipana. Anashinda gym kwa sababu yako ili u enjoy ukiwa nae.

Simon ndio mvulana anaye julikana na rafiki zako wengi kwa kua ndio mvulana ambaye unashinda nae muda mrefu. Hivyo umemuaminisha kua unampenda yeye peke yake. Kisa ni handsome

Simon ndio mvulana ambaye unaweza hata kumpost kwenye mitandao lakini Caption zako za kawaida sana zisizoonyesha dalili zozote za mahusiano.

Upo na marafiki zako wapatao wanne ambao wote life style yenu ndio hiyo.yaani hata chai mnapika inatoka na ukoko na ugali hauna ushirikiano kama waumini wa Nabii Tito (hamjui kupika)

Kila mkilala mchana mnawaza usiku muende club gani au wapi kuna pub nzuri ili mlewe.

Unaishi na mama yako na wadogo zako wanasoma. Mama hana usemi kwako kwakua ukitoka kwa Sponsor Molito unamtupia laki 2.
Mama anakuruhusu ukapumzike. Na simu yako ikiita anakuletea ndani na kukuamsha kwa adabu. Kiufupi mama yako hana kauli juu yako kwakua wewe ndio tegemezi.

Shopping yako ni laki 3 kwenda mbele. Hurudii nguo mara tatu. Usisikie simu mpya imetoka. Tayari unayo. Kwenu hamna gari lakini umeshajifunza na unatembelea magari Zaidi ya matatu lakini huna kadi hata moja.

Umepanga nyumba nzima na huna kazi mjini. Ofisi yako ni simu na sauti nzuri ya kutokea puani.makalio yako ndio mtaji wako

Miaka haisubiri. Ulikua na miaka 20 na miaka saba baadae unakua na miaka 27.

Hushtuki. Poda zinaanza kudunda na vipodozi vinaanza kukataa kushika kwenye ngozi yako.
Unaamua kubadilisha cream na kutumia zile kali kali ili ngozi ikubali.

Unakua mweupe sana. Macho nayo yanapoteza nuru. Huwezi tembea kwenye jua kali. Muda wote kope za bandia ndio mlinzi wa muonekano wako.

Sponsor Molito nae anahitaji kuwa na watoto wabichi wa miaka 20. Wewe age imeshakutupa mkono. Anakuona wa kawaida. Huna maajabu tena.

Anakuacha na kukupa wakati mgumu wa kutafuta Sponsor mwengine.

Inakua ngumu kuwapata kwa natural face, unaanza kufanya photoshoot za nusu uchi na editing nyingi ili wachuuzi wanase.

Stress zinapanda unaanza kumlazimisha Simon akave nafasi ya Molito. Simon hana uwezo. Unampiga chini unabaki na Serengeti boy wako John.

Huyo anapendwa na wasichana wengi, unamfumania na kuachana nae kwa matusi.

Unabaki Single, huna danga wala bwana. Rafiki zako ukiwapigia simu ni vizinga tu na kuwaomba wakutoe out.. huna Ishu. Unalala tu usiku wakati ulikua unajiita POPO.

Huwezi panda daladala kwakua mtaani unaitwa Cash Madame. Unaanza kupanda pikipiki kila mahali uendapo. Huna pesa za kulipia usafiri kila siku. Hivyo kuna mda jion kondakta au. Boda Boda anautumia mwil wako

Unaamua kumpa penzi Mangi wa dukani ili vitu vidogodogo uwe unachukua bure,unamtaka baba mwenye nyumba ili uishi bure

Unakuja Kutahamaki. Unafungua friji kuna maji tu, dawa ya meno imeisha, Gesi imaisha, luku nayo inakaribia kuisha, dukani kwa shirima mnadaiwa laki 2. Kodi ya nyumba inakaribia. Unamuita baba mwenye nyumba unampa penzi. Anakuongeza miezi mitatu……

Kuja kutahamaki wewe unaishi kwa kufanya mapenzi na kila aina ya mtu kwakua tu umeamua ku fake maisha yako.

Tuendelee......

Yanini yote dada zangu?
Jikubali kua wewe unaweza kutoka kimaisha na kuisaidia familia yako kwa njia salama kabisa bila kuutumia mwili wako.

Hayo madanga huwa hayazeeki bali wewe unayedanga ndio unapitwa na wakati.
Hayo madanga wanapenda wasichina wenye miaka ishirini.

Wewe ukipita basi atatafuntwa mwengine. Utaishia kutunza makabati ya kichina wenzako wakiolewa na wewe ukabaki na uzuri wako wa dukani.
Badilikine wenye tabia hii.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz