LEO NIONGEE KUHUSU MARAFIKI WA MUMEO - EDUSPORTSTZ

Latest

LEO NIONGEE KUHUSU MARAFIKI WA MUMEO

LEO TUOMBEE MARAFIKI ZAO.
Hili ni eneo ambalo Waume zetu wanahitaji Mungu sana. Wanaume wengi walikua wazuri tu lakini walipokutana na watu fulani wakaharibikiwa. Nilipoolewa kuna watu niliwafuata kabisa physicaly nikawapiga marufuku kuja nyumbani kwangu na kuhusiana na mimi au mume wangu. Na walipokuja kwa nguvu niliwafukuza. Na mpaka leo wananichukia lakini sijali maana nyumba yangu iko salama. Mengine niligundua physically hayaondoki kwa sababu shetani ameyaweka strategically kuharibu ndoa yangu, huduma, watoto na familia kwa ujumla. Haya niliyachapa kwenye maombi mpaka yakakimbia yenyewe na Leo marafiki wote walioko kwenye maisha ya Mume wangu ni marafiki wazuri wa faida na baraka. Wewe mke ni mlinzi usikubali chochote na yeyote wa kuleta UHARIBIFU aingie nyumbani kwako. Wakati mwingine ukimwambia mume wako hatari unayoiona anaweza asielewe na akawatetea, na pengine akaona unampangia maisha. Isikukatishe tamaa. Piga kote kimwili kama unaweza na kiroho pia.
1)Omba Mungu amletee mume wako marafiki wa faida watakaomfanya kuwa bora zaidi. Mithali 27:17
2)Mungu ampe marafiki watakaosimama nae siku zote katika shida na raha. Rafiki watakaompenda na kuwa pamoja naye hata wakati wa matatizo. Mungu aondoe marafiki ambao ni parasites. Wale ambao wapo kumla tu lakini akipata shida hawana msaada. Mithali 17:17, Zaburi 38:11
3)Kila rafiki anayejifanya rafiki kumbe ni adui, mfitini na msaliti anamuharibia mumeo na kumfanya mawindo Mungu amuondoe kwenye maisha ya mumeo haraka. Ayubu 17:5, Zaburi 41:9
4)Mithali 13:20 Mungu ampe Mumeo marafiki wenye hekima ili aendelee kuwa na hekima. Aondoe marafiki wote wapumbavu na waovu wanaompoteza na kumshawishi ubaya
5)Mungu afungue macho yake awaone wale wasiotakiwa kuwepo kwenye maisha yake na Mungu ampe ujasiri wa kuachana nao
6)Pray that God will surround your husband with Godly friends.
7)Pray that your husband will not hang out with people who belittle the things of God but those that delight in the word of God and in doing the right things.
8)Omba Mungu aondoe marafiki wote ambao watamtoa kwenye kusudi kwa ushauri mbaya
KATIKA JINA LA YESU, AMEN
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz