JIFUNZE JINSI YA KUISHI NA MAPENZI MWENYE HASIRA. - EDUSPORTSTZ

Latest

JIFUNZE JINSI YA KUISHI NA MAPENZI MWENYE HASIRA.


Habari za wakati huu mpendwa msomaji wa safu hii ya mahusiano nilikaa nikafanya uchunguzi ni kwanini wanaume wengi wanashindwa kumudu hasira za wapenzi wao na matokeo yake wanaishia pabaya hembu leo tuangalie machache kati ya mengi unayotakiwa kufanya kwa mwanamke mwenye hasira.

Unatakiwa kuangalia hiyo hasira yake imesababishwa na nini. Labda ni wewe ndiyo umesababisha kutokana na kukosekana na maelewano mazuri baina ya kitu anachohitaji na unachohitaji wewe kifanyike. Kaa naye na zungumza naye kwa upole si hasira kwa hasira italeta hali mbaya baina yenu.
Omba msamaha bila kujali nafasi yako ya uanaume. Kama umekosea usikatae kosa muombe msamaha nakiri kosa lako kuwa hutarudia tena. Usimfanye akapandisha hasira zaidi na kuongea visivyofaa mkafika mahali ambapo hutaweza kuhimili.


Kuwa mpole katika kipindi ambacho unamuona kuwa mpenzi wako amekasirika. Kwa sababu akiongea na wewe ukaongea kwa hasira hakutatokea maelewano bali makwaruzano zaidi


Mtumie ujumbe wa mapenzi zaidi ya zile jumbe alizozowea kuzipata kutoka kwako. Msifie mara kwa mara na ajisikie vizuri pale ambapo ana maumivu ndani ya moyo wake
Mtanie tanie utani wa kawaida ili kumrudisha katika hali ya kawaida ili ajisikie afadhali na kupunguza hasira zake na mtaweza kudumu katika mapenzi yenuKwa kuzinga niliyokueleza hapo juu utaweza kumudu kuishi na mwanamke mwenye hasira na kujikuta mnaweza kuepukana na uamuzi ambao utaleta hatima mbaya ya mapenzi yenu.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz