JE, WEWE NI MTU WA KUACHWA ACHWA, KAA CHINI, TULIZA AKILI NA SOMA HAPA! - EDUSPORTSTZ

Latest

JE, WEWE NI MTU WA KUACHWA ACHWA, KAA CHINI, TULIZA AKILI NA SOMA HAPA!


mahaba
Wakati mmoja uliopita nilikua naongea na Dada mmoja, alikua analia, anamlaumu mpenzi wake, baada ya miaka mitatu jamaa alikua amemuacha na kuamua kuoa mwanamke mwingine. Dada alikua analalamika na alikua anamaani yule Kaka. Alianza kunielezea stori yake, aliniambia tabia zake na tabia za jamaa yake, jamaa hata hakumkosea, hakumsaliti na wote walikua vizuri.
Baada ya kumalizia kuniambia nilimuuliza. “Unauhakika hicho ulichoniambia kuwa ni cha kweli?” Alinijibu ndiyo, kisha akaendelea kulalamika, akitegemea nitakua upande wake nilimjibu. “Hata kama mimi ndiyo ningekua huyo jamaa yako nisingekuoa, tena jamaa yako mvumilivu sana mpaka kuishi na wewe miaka mitatu, mimi hata mwaka nisingemaliza na wewe!”
Alikasirika na kukata simu, sikujali kwani haikua mara ya kwanza kumshauri mtu na akanikatia simu. Lakini pia nilijua kuwa nilazima atanipigia tena, hilo nilikua na uhakika nalo. Ulipita mwezo mmoja alinipigia tena na kuniomba samahani, nilimuambia bila samahani, aliniambia alikua na hasira na sasa alitaka kujua ni kwanini nilimjibvu hvile.
Nilitabasamu na kumuambia “Wewe sio kwamba una matatizo, unatabia mbaya au ni mbaya, hapana, ni mwanamke mzuri, tena unajua kupenda na kwa watu wengine kusikia mwanamke kama wewe ingekua kama baraka, lakini kisaikolojia na kiuhalisia wa maisha nikuwa wewe unaboa, unaweza kufaa kwa muda lakini ni wanaume wachache sana ambao wanaweza kukuvumilia na kukufanya mke!”
Aliniliza kwanini nikamjibu. “Subiri nimalize, nitakuambia kila kitu, naomba uniulize maswali mwishoni.” Kisha nikaendelea. “Wanawake wanaweza kuvumilia mwanaume mwenye tabia kama zako, wanavumilia si kwakua wanakua na furaha lakini kwakua hawana namna. Labda nikufafanulie ili ukiingia kwenye mahusiano mengine usiaharibu.
Una matatizo kama manne hivi amabyo ndiyo yamepelekea huyo mpenzi wako akuache. Tatizo la kwanza nikuwa unataka kutumia muda wako wote na mpenzi wako hivyo unalazimishia nayeye atumie muda wake wote na wewe. Unampenda sana moenzi wako na baada ya kuona nayeye anakupenda anakutoa out mnakua pamoja basi na wewe ukaona ndiyo raha, ni vizuri kuwa pamoja.
Mwanzoni alikua ana enjoy kwani mlikua ndyo manaanza, alikua hajakuchoka, hajamjaanza kuboana. Lakini sasa ikawa ni kila siku, kila mkitoka uataka kuwa nayeye, akitoka kazini unataka kuwa na yeye, weekend zote unataka kuwa na yeye, mbaya zaidi nikuwa hata kwenye simu unataka kuchat nayeye. Anapotumua muda mbalia na wewe unalalamika, unashutumu, unahisi kama anakusaliti na unakua na kisirani.
Kama akitoka kazini hajakuambia unalalamika, akitoka na marafiki hajakuambia unalalamika. Lakini kama mmetoka na marafiki, halafu ikatokea akakaa mbali na wewe, akawa anapiga stori na marafiki zake badala ya wewe unanuna na unahisi kakudharau. Hapa baadhi ya wanawake tena si wote kwani wengi nao wanaboreka wanaweza kuvumilia, lakini hakuna mwanaume anayeweza kuvumilia.
Nilazima umpe mpenzi wako nafasi, umauche akumiss, atamani kukuoana, atamani kukupigia simu. Lakini wewe hata ukimuona online, ukatuma mesejia sipochat ana wewe utalalamika na kuona kama kakudharau, kama alikua anachata na wengine. Mwanaume ni lazima akuchoke kwani kila muda unamhitaji yeye na yeye anakosa hata muda wa kuwa peke yake unataka awe na wewe kila mara.
Kwa kifupi unapomganda mwanaume hata kama umzuri vipi, hata kama unamganda huku ukimlamba miguu lazima akuchoke na hii ni sababu kubwa watu wengi wanaachika na sababu kubwa kwanini umeachika, alishakukinahi kwani Kuku na utamu wake kila siku ukimla kila siku basi anaboa. Lakini pia unapokua naye kila mara, lila mahali unamruhusu kuona na kuchukia vitavia vyako vingi vidogo vidogo vivay amabavyo asingeviona kama msingekua karibu kihivyo”
Aliuliza uliza maswali lakini mwisho alikubali kuwa ndivyo alivyo na kweli yeye alidhani kuwa ni mapenzi hakujua kama anaharibu. Nilimuambia sio yeye tu, wengi hudhani kutuma meseji kila saa, kumganda mwanaume na kuacha kuwa na maisha mengine ndiyo kushikilai pendi. “Sababu ya pili ya wewe kuachika nikuwakua huna marafiki, huna watu wengine zaidi ya yeye, huna watu wa kupiga umbea na mambo kama hayo.”
Nilimuambia “Wanawake wengi wanapokua katika mahusiano siriasi huanza kusahau marafiki, labda wana marafiki ambao hawawaamini hivyo huwaweka mbali na wapenzi wao. Kuna wale ambao husema mimi siwaamini wanawake ni wambea. Kwa maana hiyo rafiki yako mkubwa ni mpenzi wako, hii ikimaanisha kuwa, unapokua na umbea unataka kumuambia yeye, unapokua na mawazo unataka yeye akufariji.
Sasa hapa kuna mambo mawili, kwanza nikuwa si kila wakati mwanaume atataka kusikiliza umbea wako, umbea mwingine unatakiwa kupiga na mpenzi wako, lakini jambo la pili nikuwa wakati ukiwa na mawazo, unahitaji mtu wa kukufariji basi uutataka kuongea na yeye. Lakini kama yeye ndiyo alikusababishia yale mawazo utajikuta huna wa kumuambia, unakaa nayo na unajikuta unakua na hasira.
Kitu kidogo, kosa dogo unaliona kubwa sana kwakua tu hujapata mtu wa kuobfea naye ukaondoa mawazo. Unajikuta unakasirikakasirika na kuwa na kisirani, hapo moja kwa moja unaboa hata mtu kuwa karibu na wewe. Unaanza kuwa mtu wa kulalamika, na baada ya muda anachoka kule kulalamika kwako, anakuchoka na wewe na moja kwa ,moja anakuacha.”
Aliendelea kuniuliza maswali, kwake aliona kama ni mambo mdogo lakini kiuhalisia ni makubwa, nilimuelewesha na kuendelea. “Huna maisha yako unaishi maisha yake.” Hapa nilitulia kidogo kwani nilitaka aelewe vizuri. “Baada ya kumpata huyu mwanaume, ukaona anakupenda, mapeana ahadi nyingi ukajikuta kama unakua mke wake, unaanza kufanya kila kitu kama mke wake.
Kwanza ilianza kuhusu kazi, mwanzoni ulipata kazi sehemu flani lakini ukakumbuka alishasema haipendi. Hakukuambia uache lakini ukaacha nayeye akajua, lakini ulipopata kazi badala ya kufanya maisha yako ukawa unafanya maisha yake, uliendelea kubaki nyumbani kwenu kila siku ukimuambia huwezi kupanga mpaka uolewe.
Haikuishia hapo, ulianza kuwa mke wake, ulianza kumshauri mambo mengi, ukaanza kumchagulia kila kitu, kila kitu anchotaka kununua wewe ulimshauri vile vitu unavyopenda na unavyoona kama ukiwa mke utacvitumia vizuri. Kwa mfano,. Alipotaka kununua jiko la gesi la kawaida ulimuambia ni vizuri akanunua na lenye Oven akitaka kupikia keki sijui na vitu gani wakati yeye alitaka lakuchemshia maji tu.
Ulishajiona mke wkake hivyo ulitaka anunue vitu ambavyo wewe kama mke utavitumia. Lakini pamoja na wewe kuwa na hela ukawa hufanyi vitu vya maendeleo, akitaka kununua kiwanja unamshauri kununua sehemu ambayo wewe unapenda kuishi, TV ambayo unapenda wewe, mapazia yale unayoipenda wewe, Zulia unalopenda wewe. Akikataa unalalamika mpaka basi kwani unaona kama hakusikilizi.
Kwakua ulishajipa hadhi ya mke basi asipokusikiliza unaona kama kakudharau mkewe kumbe yeye bado hajawaza huko. Bila kujijua unaanza kuwa kisirani, unaanza kumkalia na bila kujijua unajikuta unamkera kwakua wewe hauna maisha yako, mawazo mazuri unayomshauri wewe huyafanyii kazi hivyo badala ya kukuona mshauri basi hkuona kama unataka kumpangia maisha yake na kumkalia kichwani.”
Alishangaa lakini nilimuambia hizo kwa yeye (kila mtu ana stori yake) ndiyo ilikua sabbau ya kuachwa hivyo kama na wewe ni mtu wa namna hiyo, hembu mpe pumzi mpenzi wako, usitake kutumia muda wote wa zaida na yeye, hata kama ni mumeo au mkeo, atakuchoka mapema kama kila saa mko naye, kila saaa unataka mhat naye. Tafuta marafiki wa kukupunguzia stress na kama uko kwenye mahusiano basi kuwa na maisha yako acha kuwa mke kabla ya kukuoa.
Kama wewe ni mtu wa kuachwa achwa, upo huna mpenzi kabisa, hembu kabla ya kuanzisha mahusiano mengine, chukua kitabu changu cha “ndoa Yangu Furaha Yangu” soma sehemu ya nne. Jifunze namna ya kujipenda na kuwa na furaha yako mwenyewe kisha utaona hata wengine watapenda. bei yake ni shilling elfu kumi tu. Unalipia kwa M-Pesa No. 0742-381-155 au Tigo Pesa No. 0657-552-222 na kitabu unatumiwa kwa Whatsapp/Facebook/Email.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz