JE NI SAHIHI MKE NA MUME KULALA HUKU WAMEVAA NGUO ZAO ZA KUSHINDIA? - EDUSPORTSTZ

Latest

JE NI SAHIHI MKE NA MUME KULALA HUKU WAMEVAA NGUO ZAO ZA KUSHINDIA?

Image result for tendo la ndoa asubuhi

UCHI BILA HAYA

Mwanzo 2:24-25

"Kwa hiyo Mwanaume atamwacha Baba yake na Mama yake ataambatana na Mkewe , nao watakuwa mwili mmoja.
Nao walikuwa uchi wote Wawili , Adamu na Mkewe , wala hawakuona haya."

Yapi ni mavazi sahihi kwa Wanandoa wakati wa kulala usikulicha ya kulala kwenye kitanda kizuri ama cha kawaida, namna ya ulalaji imekaaje je kulala na nguo ama kama walivyozaliwaUnakuta mfano; Mume na Mke wamelala; Mume katinga jeans, bukta, chupi. Mke nae katinga chupi, skin tight, jeans bado wamejifunika kila mtu shuka zitoWapo wanaovaa track suite za kulalia, wapo wanaolala uchi kabisa, wapo wanaovaa chupi/boxer tu, kuna Wanawake wanalala na kanga na chupi ama moja wapo tu, n.k.

Yote hayo yapo ndani ya ndoa zetu na ni kipimo cha upendo kupoa ama kuwa motomoto.

CHUKUA HII KUTOKA KWANGU:😁😁😁😁
Waswahili wanasema ukikubali kuolewa sharti ulale bila nguo kabisa.....msemo huu una maana kubwa kwa ustawi wa ndoa zetu.

Unajua maandiko yanatuambia Mume na Mke ni mwili mmoja kwani Mwanamke ametokana na ubavu wa Mwanaume
Tupitie andiko hili kisha tuendelee...
Mwanzo 2:18,20-25 "Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.
20 Adamu akawapa majina yao kila mnyama wa kufugwa, na ndege wa angani, na kila mnyama wa mwituni; lakini hakuonekana wa kumsaidia Adamu aliyefanana naye.
21 Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake,
22 na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya Mwanamke, akamleta kwa Adamu.
23 Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.
24 Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.
25 Nao walikuwa uchi wote wawili, Adamu na mkewe, wala hawakuona haya.

Hivyo basi ikiwa kweli Mume na Mke wanapendana kwa dhati na hawataki kuchokana sharti walale kama walivyozaliwa ili KUPEANA JOTO LA MAPENZI.

Siyo joto tu bali ule ukaribu wao unamfanya Mwanaume kukamilika yaani anakuwa karibu na ubavu wake ambao ndiye Mkewe na Mke anakuwa sehemu yake salama maana hawezi kujitegemea maana ni sehemu ya mwili wa Mumewe.

Lakini pia tunaona wote wawili walikuwa uchi na wala hawakuona aibu mpaka pale walipoasi kama ilivyo kwa Mume na Mke ambao uanza kulala na nguo ama kujificha pale wanapopoteza ushirika wao.

Muhubiri 4:9-12
inasema "Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; Maana wapata ijara njema kwa kazi yao.
10 Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua!
11 Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje kuona moto?
12 Hata ikiwa mtu aweza kumshinda yule aliye peke yake, wawili watampinga; wala kamba ya nyuzi tatu haikatiki upesi".

Hapo maandiko yameweka wazi kabisa kuwa mnapokuwa Wawili kama Mwili Mmoja yaani mmeunganishwa kwa upendo na mahaba hakuna wa kuwashinda.

Joto lenu lina nguvu ya upendo udumuo( everlasting love).Hakuna anayeweza kumfanya mwenza kuchepuka wala wala kushindwa kujiepusha na tamaa huko nje kwani joto lenu lina nguvu ya upendo na mshikamano.

Makahaba wanaweza kumshinda mtu mmoja lakini mkiwa wawili kama mmoja hawawezi.Umoja wenu ni nguvu tosha dhidi ya michepuko huko nje na tamaa ya mwili.

Hivyo basi tambua umuhimu wa mavazi sahihi kama vile kitenge ama khanga laini tena yenye mvuto kimahaba ama taulo kwa mwanaume ama night dress muwapo faragha maana siyo lazima kuwa uchi wa mnyama kama mnawanga vile.
Mpe nafasi mwenza wako kupata joto la penzi lako na kuuona ukamilifu wake.
Usikubali kumchoka mwenza wako hata kuweka mipaka kwa mavazi magumu yanayosababisha arudi kwenye upweke kama tulivyoona katika mistari tuliyoanza nayo ambapo tunaona ADAMU ALIONEKANA MPWEKE pasipo mwanamke.

Tambua kuwa siyo Mwanaume tu anayeweza kuwa mpweke bali hata Mke anaweza kuwa mpweke ikiwa utapuuza joto lake na kumwacha peke yake.Tunaona Eva alipata nafasi ya kudanganywa na nyoka kutokana na kuwa peke yake.Kama Adamu angekuwepo naye wasingeweza kudanganywa maana Adamu alilijua kusudi na wajibu kuliko Eva.

Mume kuwa na kimbelembele kwa mkeo, wakati wote mvute na kumuweka karibu yako maana ndiye ubavu wako na bila yeye haujakamilika.Kadhalika Mke jionyeshe umekubaliwa na Mumeo kama msaidizi pekee wala msimpe shetani nafasi.
Mnalala na nguo kisa tu mnaona kama hakuna haja ya joto la mwenzako.Tambua joto lake ni zaidi ya nguo,shuka ama blanket unalojifunika kufukuza baridi na UPWEKE.

Tena nawakubali wale Wanandoa ambao wanapolala mikono yao uwahifadhi vyema wenza wao.Hata ikitokea kamkuta mwenza wake kalala basi atambusu na kumkumbatia na kudumisha upendo kwa joto lake.

Wanaume wengine wakilala hawawezi kupata usingizi kama hawajawashika wenza wao kifuani,kiunoni,nywele n.k.Yaani wanamiliki mali zao 100% nje ya hapo usingizi hauji.

Hata ikitokea Mke anataka kuamka lazima ashituke maana hawezi baki mpweke.

Kadhalika Wanawake wanaojua mahaba hawawezi kupata usingizi kama wenza wao hawajarudi yaani watapiga simu na kuona upweke mpaka mwenza wake arudi tena akiwa salama.

Tena wakati wote atavaa nguo zenye mvuto na hauwezi kuwakuta na nguo za ndani unless otherwise wapo katika siku za Wanawake na Mume anakuwa anajua hilo.

🔴NDOA NA IHESHIMIWE NA WATU WOTE ðŸ™
NA MALAZI YAWE SAFI ðŸ™
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz