JE! MWANAMKE MZURI YUKO VIPI?


Image may contain: 1 person
Kila mtu anaweza kuwa na majibu tofauti pale anapoulizwa uzuri wa mwanamke ni nini? kuna atakayesema uzuri wa mwanamke ni muonekano wake, yaani umbo lake zuri la kuvutia, sura yake, miguu nk, lakini pia yupo atakayesema uzuri wa mwanamke ni kuwa na tabia nzuri ama uzuri wa mwanamke ni kujituma na kufanya kazi kwa bidii.

Majibu yote yanaweza kuwa na mtazamo tofauti, lakini ukimfikiria mwanamke mzuri ni yule ambaye anajitambua na kufahamu umuhimu wake katika jamii, mwanamke mzuri ni zaidi ya urembo wa sura yake, ama muonekano wake kumbuka sura nzuri haiwezi kudumu milele, kwani kuna siku itachoka na kuzeeka, muonekano wa mwili na wenyewe hubadilika siku zinavyozidi kwenda hata kama ufanye nini lakini mabadiliko katika mwili ni sehemu ya maisha ya binadamu, ila mwanamke ambaye ni mzuri kutokana na tabia yake, yaani mzuri kutoka moyoni siku zote atabaki kuwa mzuri haijalishi mabadiliko ya muonekano wake.

Mwanamke mzuri mbali na kuwa na ujanja wa kuchagua vipodozi urembo kujipodoa na nguo za kisasa, huwa na akili ya ziada kuhusu maisha hususani ujasiriamali na maendeleo hivyo kumfanya kuwa msaada mkubwa kwa mume katika kujenga maendeleo ya familia, mwanaume siku zote ni kama injini inafanya kazi kwa nguvu ila inahitaji kupoozwa kwa hiyo mwanamke mzuri sikuzote humfariji na kumshauri mume njia rahisi na mbadala ambazo huenda zikasaidia katika kuzitatua changamoto za kimaendeleo sio kila siku mwanamke anaongea umbea na udaku tu.

Mwanamke mzuri ni mwanamke anayemjua Mungu na anaishi akiwa na hofu ya Mungu, vilevile ni mvumilivu, mpole, na anayejua kuishi na watu mbalimbali wanaomzunguka katika maisha yake ikiwemo wakwe na ndugu wa mmewe . Mwanamke mzuri sikuzote anajikubali katika hali yoyote iwe ni katika shida au raha, siyo muongo ni mkweli katika maisha yake na wakati wote anasimamia ukweli bila kuwa na hofu. Mwanamke mzuri hatakiwi kuwa na hasira ijapokuwa ni kitu ambacho kipo katika maisha yetu.

Nakutakia USIKU mwema, Mungu Akubariki na kukulinda

Usisahau ku LIKE


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post