Hii ni kwa watoto wakike mlioko vyuoni - EDUSPORTSTZ

Latest

Hii ni kwa watoto wakike mlioko vyuoni


Wadogo zangu mlio chuoni, mwanaume akikuambia kuwa nitakuoa wakati Boxer aliyovaa ni nguvuya Boom au alimlilia Mama yake ndiyo akapewa basi kubali tu, muambie ndiyo lakini kwenye moyo wako jua kuwa ni uongo. Yaani wewe huna tofauti na yule dada ambaye tukiwa Kidoato cha Pili nilimuambia kuwa tuache chuo tuoane tuende zetu mjini tukale maisha!
Uko mwaka wa kwanza mshapanga na idadi ya watoto, mshaambiana kuwa ukifika mwaka wa tatu ubebe mimba ili mkimaliza mnoana! Dada yangu wapo wanaoona kweli lakini angalau mwanaume awe na uwezo wa kununua Boxer kwa pesa yake, pesa aliyonunua kwa jasho lake. Tofauti na hapo ni kudanganyana.
Halafu kuna kale katabia mkiwa chuoni mnawaona wale waliomaliza chuo amabo hawana kazi kama ni wajinga flani. Unaanza amenaimbia kuwa akimaliza atarafuta kazi, akikosa atajiajiri kisha tutaanza kuishi pamopja! Dada si kirahisi namna hiyo, huyo mwanaume akija akipigwa na jua la mataani mahaba yote yanageuka jasho, yanatoka tena kwa kununa wewe unaachwa na Mimba yako.
Najua unajisikia raha tena unabana na pua kabisa “Mimi kashanipeleka na kwao!” Tena hapo unatakiwa kuwa makini sana, sana sana, kama una mwanaume ambaye hana kazi, yupo chuo anakupeleka na kwa, unakutana na Mama yake, unalala kwao hata kwenu hawajui na huyo Mama mkwe anakuchekea unaiotwa mke kabisa basi hiyo familia nayo ni shida, kuwa makini aisee.
Kama mpaka hapa hujaelewa, unadhani wakwako ni tofauti kisa kakusuprize kakubalisha pete, unaringa mwenyewe, aisee subiri huyo mwanaume apate pesa. Huwezi kusema mwanaume anakupenda kama hana, pesa, hapa sizungumzii utajiri wa kumiliki nyumba na magari, hapana, nazungumzia pes aya kupanga chumba kimoja, kununua chakula na kuweza kuhudumia mke, kama bado hizo anaomba basi huyo hajaanza kupenda.
NB: Nishamaliza ukubali ndiyo hivyo ukatae ndiyo hivyo, malizeni chuo kwanza, anzeni maisha kama bado mtakua mnapenda basi mtaoana.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz