HAWA NDIO WANAWAKE, LEO NATOBOA TU - EDUSPORTSTZ

Latest

HAWA NDIO WANAWAKE, LEO NATOBOA TU

Wasichana wengi mmekuwa na kilio kikubwa sana kuhusu mahusiano yenu, na mnadai hamna imani na wanaume kabisa, jambo ambalo ni hatariiiiiii sana, sasa hebu tuangalie jambo moja hapa.
Kila siku nipo nanyi nikijaribu kutafakari jinsi gani niwasaidie ili pengine kunusuru hali ngumu za mahusiano, lakini leo ninalo jambo kwenu.
Kwa siku hizi kadhaa nimejifunza kwenu jambo ambalo sijaweza kukaa nalo, nimeona Ngoja niwaambie hapa hapa kabla hamja haribikiwa.
Najua wanawake wengi mnaomba Mungu awape waume wema lakini ninyi hamko tayari kuwapokea hao wanaume wema, mnatumia akili zenu kupata waume ambao mwisho hawawafai mwisho mnalalamika na kuwadharau wanaume wote na wasio na hatia.
Mfano kuna wanaume ni wapole, wanajua thamani ya Mwanamke, wanajali na ni wenye hekima, wanajua mtahitaji ya Mwanamke, ni wacha Mungu, wanajua kubembeleza kwa maneno safi, na ni wepesi kuhifadhi madhaifu ya Mwanamke. Lakini wanaume hawa unakuta hana uwezo mwingi kifedha. Nimesikitishwa sana kuona kuna wanawake au Mabinti wengi kuona mkidai na kuhoji kwamba tena kwa dharau kuwa et
je Mtakula hayo maneno matamu?
Je, maneno yake ya upole yatawapeleka saloon?
Je, upole wake utakuwa chakula?
Mkimaanisha kuwa hayo hayana thamani kwenu, ila zaidi sana Mwanamume mwenye pesa ndiye mwenye tija kwenu.
Mnataka Wanaume wenye pesa, wenye uwezo wa kuwapeleka saloon, wa kuwapa chakula kizuri, kuwalaza pazuri, kuwapa nguo nadhifu nk. Lakini mwisho Wanaume hawa hawajali uwepo wa mke, hawajui kushuka kwasasabu ya kiburi cha pesa zao, wanawawatelekeza na mwisho mnaanza kuwadharau Wanaume wote wakati wengine mnawaonea tu.
Mwisho ndio maana hata maombi yenu yanaonekana hayana maana, mkiomba Mungu anawapatia lakini wakifika hao wanaume wema, mnawapima kama wanaweza kuwahudumia, kama hawana mnawakataa maana yake umekataa chaguo la Mungu kwako ila unaingia kutafuta mwenyewe unayeona atakufaa kwa kigezo cha mwenye unafuu wa maisha.
Upendo wa dhati unaficha madhaifu yenu ndani, pasipo upendo pesa ya kazi gani?
Anakupenda na hana uwezo basi mpokee na umpe ushirikiano kisha msaidiane kutafuta maisha, mnataka maisha yaliyo andaliwa na nani?
Mnataka anayekuoa awe tayari anapesa, je hizo pesa ametafuta na nani? Una amani gani kusubiri ule ambacho haujatafuta?
Unataka mwenye maisha mazuri je alitafuta lini? Ulivyoishi wewe na yeye hivyo hivyo, kama wewe hauna yeye anawezaje kuwa navyo?
Kuwa mwanamke haimaanishi unahitaji kutunzwa kama sahani iliyopo kabatini, na mtachelewa kuolewa au mtaumizwa kwa kigezo cha kusubiri wanaume wenye uwezo na si wenye upendo wa dhati.
Leo mnauliza mtampataje mwanamume mwenye upendo wa dhati? Si kwamba hamuwaoni ila kuna shida kwenye kukubaliana na hali zao za maisha, mnafika mahali mnaamini kuwa upendo unaoneshwa kwa pesa na ndio maana mwisho mnadaiwa Ngono kabla ya Ndoa na mnashindwa kukataa kwasababu tayari mmekuwa watumwa wa pesa za hao wenye nazo.
Pesa ni jambo nyeti sana katika mahusiano lakini pakiwa na upendo wa dhati.
Wewe unayesoma post Hii leo, Mungu ameshakupatia mume inawezekana umeshatoka kumkataa unamtafuta wa kwako mwenye unafuu wa maisha kwa macho yako amini umeumia, rudi kamfuate mpendane mtafute maisha.
Inawezekana yupo njiani anakuja jiandae kumpokea bila kuweka kipaumbele cha umaskini wake. Siku zinabadilika mnaweza pendana na mkajatafuta mkawa wenye uwezo kuliko waliorithishwa vipato vyao.
WITO WANGU LEO KWAKO!
WANAUME WENYE UPENDO WA DHATI WAPO ILA HAWANA UWEZO, NA HAKUNA FAIDA KWAKO KUWACHUKIA WANAUME MASKINI WENYE UPENDO KWASABABU YA WANAUME WENYE UWEZO WASIO NA UPENDO!
NASEMA TENA MSIPOBADILIKA, MTALIA NA KUISHIA KUSEMA MUNGU AMEWASAHAU NA KUWACHUKIA WANAUME WOTE KUSIKO WASAIDIA, HAKUNA WA KUWAFUTA MACHOZI.
Kama umejifunza chochote hebu Share umsaidie na rafiki yako, Follow page ili kupata masomo mengine zaidi.
Mtia Moyo
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz