HATMA YA MAHUSIANO YAKO NI NINI?: - EDUSPORTSTZ

Latest

HATMA YA MAHUSIANO YAKO NI NINI?:


👉Kudate ni jambo rahisi sana, Ila kuna siku ukiwaza na kutafakari kwann unadate utajikuta umeshapoteza muda wako, pesa zako na hata kupoteza muelekeo wa maisha kwa mtu ambae hujui kwann ulikuwa nae wala kwa Lengo gani?
👉Katika kizazi cha Leo ukiondoa mapenzi 'sex' katika mahusiano Utagundua kwa asilimia kubwa ya wanaume hawana jambo lingine la maana kuwafanya wawepo kwenye mahusiano, Vile vile ukiondoa Pesa 'Utajiri' katika mahusiano Utagundua asilimia kubwa ya wanawake hakuna jambo lingine wanalohitaji kwenye mahusiano.
👉Kizazi cha sasa Bila pesa asilimia kubwa ya wanawake wataona haina haja ya wao kuwa katika mahusiano na Bila Sex wanaume wataona haina haja ya wao kuwepo katika mahusiano. Wanawake wengi wanalalamika sana kwamba wanaume wanapenda sana sex akishakufunua mara mbili tatu basi ule upebdo wa mwanzo unapungua. Hivyo hvyo wanaume wanalalamika sana kwamba wanawake wanapenda sana pesa inamaana wakishazipata wakizitumia na zikiisha basi wanakuhama hakuna mapenzi ya mwanzo tena hutafuta mweny pesa, Hii ndio hasara ya mahusiano.
👉Hatma yako ya mahusiano ni nini, Jiulize jee nitatumiwa mpka lini, nitaolewa na nan kwa mtindo huu, kijana jiulize jee pesa zangu zitatumika mpka lini, jee nina mpango gani wa kuwa na maendeleo, jee ninahitaji familia na jee nitaitunza vipi kama pesa yangu inatumika kununua mwili wa mtu ili kukidhi haja ya muda mfupi. Usiingie kwenye mahusiano bila malengo ndugu yangu, Utakuta unapoteza muda kwa mtu ambaye siye.
👉Kabla hujafikiria kuwa na mtu fulan yatathimini maisha yako. Fikiria unatakiwa kuwa mme au mke wa mtu, unatakiwa kuwa baba au mama wa familia, Jee huyo uliye naye ndiye mwenza wako sahihi au unajiegeshe tuu ili maisha yasonge. Jee ndiye mzazi mwenzio, Jee ndiye mkeo au mmeo mtarajiwa. Usikae tuu na mtu ili na ww uonekane upo kwenye mahusiano, Kaa na mtu kwa malengo. Epuka mahusiano ya kujiegesha, mahusiano ya Kuiga, mahusiano ya kujionyesha yatakusababishia majuto.
👉Ni wakati wetu sote kubadili mtazamo, mahusiano yamekuwa fashion kila mtu analia na upande wake, wanaume walia wanawake wanapenda pesa japo sio wote ila asilimia kubwa pesa imekua kupaumbele katika mahusiano, na vile vile sex imekuwa kipaumbele katika mahusiano.Tujifunze kuongeza thamani katka mahusiano. Ikumbukwe mahusiano sio starehe tuu, Bali ni kupeana mbinu za kimaisha na kujua nn mnataka kufanya katk umoja wenu, mmekutana ili nn mioyo yenu inasema nn.
J4REAL




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz