Kila mtu hapa ulimwenguni ameumbwa na sifa tofauti tofauti. Kuna wengine wameumbwa na tabia za kuridhisha na wengine wameumbwa na tabia ambazo hazifurahishi. Hii pia inajitokeza katika wanawake. Katika mahusiano, utapata kuwa wanawake wanakuwa na tabia ambazo aidha zinawapendeza wanaume wao ama zinawachukiza.
Ok. Katika kuangalia tabia za wanawake, tumekuja na orodha ya wanawake ambao kama mwanamume unafaa kuwa chonjo nao kwani watayafanya maisha yako ya mahusiano kuwa ya balaa. Labda sahizi uko katika mahusiano ya muda mrefu na mpenzi wako ama sahizi uko mbioni unatafuta, kuwa macho na aina hii ya wanawake ambao wanaweza kukuharibia ama kukuletea shida
katika mahusiano yako nao mbeleni.
1. Mwanamke anayekuganda nguoni
Huyu ni aina ya mwanamke ambaye amekupenda kisai cha kuwa hawezi kufanya jambo lolote bila kukuhusisha wewe. Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye amekuwa amezama na penzi lako kiasi cha kuwa hakupi nafasi ya kupumua. Kila kitu atakachofanya lazima uwe karibu nayeye. Well, hii ni poa kwa mahusiano lakini itafikia mahali fulani ambapo utachoshwa na tabia zake haraka. Na pia yeye kama mwanamke atakuwa na mawazo finyu kwani kila wakati anapokumbwa na jambo fulani hawezi kulitatua bila kukuhusisha.
2. Mwanamke aliyepagawa kimapenzi
Nani hapendi mwanamke anayempenda kupindukia? Kila mtu angekuwa na mwanamke aina hii wanaume wangekuwa na furaha milele. Lakini kulingana na utafiti ni kuwa aina hii ya mwanamke ni miongoni mwa wanawake wabaya kabisa ambao wanaweza kufanya maisha yako kuwa ya taabu.
Mwanamke kama huyu ungempenda siku za kwanza kwanza lakini tatizo ni kuwa kadri siku zinavyopita mnapokuwa pamoja utagundua tatizo flani, mwanamke aina hii hangependa ufanye chochote bila yeye kuwa karibu yako. Hii inamaana kila mahali unapoenda lazima akuandame. Aidha ukiwa na marafiki zako, vilabuni, wanjani…nk, yaani kiufupi kila uendapo anataka awe hapo hapo ili akuangalie na akupende zaidi. Utamweza kweli huyu?
3. Mtumiaji
Kuna aina ya wanawake ambao wanakuona wewe kama mwanamume mzuri ili wakutumie kama chambo kuwafanikisha kimaisha. Unaweza kuwa mwanamume ambaye unauunganishi na watu wengi, ama unaweza kuwa mwanamume ambaye unapendwa na wengi. Mwanamke aina hii ataona kuwa akiwa karibu na wewe itakuwa nafasi rahisi kwake kupata connection na marafiki zako kwa
urahisi. Hii inamaana kuwa pindi mwanamke aina hii akifanikiwa kupata kile ambacho amekuwa akitafuta, bila kupoteza wakati atakutema na kukuacha kwenye giza.
4. Mwanamke asieomba msamaha
Huyu ni aina ya mwanamke ambaye hawezi kuomba msahama kwa jambo lolote ambalo amefanya hata kama ni la makosa kiasi gani. Anaweza kuomba msahamaha kwa shingo upande ama aamue kunyamaza kimya tu kwa jambo alilofanya la kukwaza ama kuudhi. Owk kwanza ni kuwa aina hii ya mwanamke anaogofya sana kwani mtu ambaye hakubali makosa yake si mtu mzuri wa kuishi naye hata mara moja.
5. Mlalamishi
Huyu ni aina ya mwanamke ambaye nyakati zote yeye hulalamikia kuhusu hili na lile. Yaani kwake hakuna jambo zuri ambalo limeshawahi kumfanyikia. Aidha atakuwa akilalamika kuhusu marafiki zake, maisha yake ya kila siku nk. Yaani yeye siku zote hana amani. Aina hii ya mwanamke haifai kabisa kwani ulalamishi wake wa kila siku utakuchosha kwa haraka.
6. Asiyejielewa
Huyu ni mwanamke ambaye haelewi anachotaka maishani. Wakati wote yeye atakuwa anahangaika na uchaguzi wake na hajiamini na chochote ambacho anachagua. Aina hii ya mwanamke achana nayo kwa sababu wewe pia inamaanisha hayuko asilimia mia moja kama aendelee kuwa nawe au la. Aina hii ya mwanamke mara nyingi huwa na wanaume wengi na nirahisi kwake kukuendea kinyume kimapenzi. So kama wewe unamahusiano na mwanamke aina hii aidha uachane naye fasta ama akuwache wewe wa kwanza.
7. Anayetawala na kutotosheka
Hii ni aina ya mwanamke ambaye anatarajia makuu kila wakati na hatosheki kile alicho nacho. Anapenda kutawala na kila kitu anataka kifanywe vile ambavyo anavyotaka yeye. Owk najua wanawake wanapenda wanaume ambao ni gentlemen, lakini baada ya muda mfupi utakuja kugundua kwamba aina hii ya mwanamke watakufanya bwegu muda unaposongea, yaani watakukalia kichwani na wao kujifanya mabosi.
8.Mwenye maoni ya ukashifu wakati wote
Kuwa na maoni na kukashifu si jambo baya kwani kukosoa mambo katika mahusiano ni jambo zuri katika maisha. Lakini usizidishe. Aina hii ya wanawake wanaokashifu kupitia kiasi ni wale ambao wakisema jambo fulani basi litabakia hilo hilo na hata ufanyeje hawawezi kujeuza. Aina hii ya wanawake watafanya maisha yako kuwa balaa kwani wakisema jambo flani, bila hata kufikiria wenzao.
9. Nusa Nusa
Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye haipiti siku bila kukuchunguza. Kila wakati anapopata mwanya anajaribu kukuchunguza mindoko yako. Unaweza kuwa mwaminifu kwake lakini yeye bila kutosheka lazima akuchunguze chunguze, mara aangalie simu yako, atake kujua umetoka wapi umeenda wapi, jana ulivaa nguo gani, anawauliza maswali marafiki zako kukuhusu nk. Owk aina hii ya mwanamke muogope sana kwani pia yeye haaminiki. Kila anachofanya yeye anashuku pia wewe utafanya. Hivyo mara nyingi ukiona mwanamke anashindwa kukuamini kwa uhusiano, inamaanisha kuwa pia yeye ana hilo tatizo, so ukiona mwanamke wako ana hizo tabia achana nayeye mara moja.
10. Asiye na maono
Aina hii ya mwanamke inafanana karibu na ile ya asiyejielewa lakini hii ni kuwa mwanamke aina hii hana maoni kujihusu yeye mwenyewe. Ukimmuliza kitu chochote anakwambia kuwa hajui ama hana mtazamo wowote kuhusu jambo lolote. Mwanamke huyu anaweza kuonekana mwanamke mzuri mara ya kwanza kwa sababu hawezi kukupinga na chochote unachosema lakini pindi muda unaposongea utaona kuwa ataanza kuwa mzigo kwako. Aina hii ya mwanake iogope sana kwa sababu anaweza kuwa anafanya hivyo maksudi huku akiwe ameweka mtego ama anamalengo yake kibinafsi kutoka kwako. Mwanamke asiyetoa maoni kuhusu chochote unachosema ni umuogope
sana.
11. Mcheza ndondi
Hii ni aina ya mwanamke amabye anakasirika kwa haraka na akichukizwa na chochote kile ambacho kinakuja kwa akili yake ni vita. Aina hii ya mwanamke sitaigusia sababu kila mtu anajua matokeo yake.
12. Mtoto wa mama
Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye hatofanya chochote bila kuingiza wazazi wake katika maongezi yake. Aina hii ya mwanamke ni mbaya kwa sababu mwanamke aina hii hata ufanye nini lazima aingize wazazi wake ndani yake. Hii inamaanisha kuwa hawezi kudhamini maoni yako kabla kuwauliza wazazi wake.
Post a Comment