ACHA KUMPA MOYO WAKO MTU AMBAYE HAYUKO TAYARI HATA KUKUPA MUDA WAKE - EDUSPORTSTZ

Latest

ACHA KUMPA MOYO WAKO MTU AMBAYE HAYUKO TAYARI HATA KUKUPA MUDA WAKE


Kila simu upige wewe na akipokea mkiongea sekunde kadhaa utamsikia “Ngoja nitakucheki baadaye” kisha anakata simu halafu hakutafuti mpaka umtafute wewe. Kila siku yuko bize kuonana na wewe mpaka anapokuhitaji anapokuwa na shida flani ambyao anataka umsaidie au umtimizie.
Yuko online lakini hajibu meseji zako ingawa anachat na marafiki zake. Hawezi kuongozana na wewe wala kukusindikiza sehmu ila akikuhitaji anataka umsindikize, tena anakupa taarifa wakati anaondoka hata sio masaa kadhaa kabla na usipoenda ni lawama na matusi.
Hakujali kwa chochote hata kukutumia meseji umeamkaje lakini bado unajipendekeza kutuma mamia ya meseji. Unamatatizo gani? Unakasoro gani? Hembu acha kumpa moyo wako mtu mabaye hata hakuthamini na kukupa muda wake.
Sisemi akupende kama unavyompenda lakini angalau akujali kama mwanadamu, akupe hata muda wake kidogo. Mtu wa namna hiyo hata ukifanikiwa kuingia naye kwenye ndoa ni mabalaa tu unajitafutia, punguza kujipendekeza na kujishusha kana kwamba unamalori ya kasoro!
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz