Tetesi za soka leo - EDUSPORTSTZ

Latest

Tetesi za soka leo

Tetesi za soka  leo february 02
Tetesi za soka  leo 

Tetesi za soka  leo 

Kiungo wa kati wa Ufaransa Tiemoue Bakayoko, 24, ambaye yuko AC Milan kwa mkopo kutoka Chelsea, amesema angependelea kusalia katika klabu huyo ya Italia. (Corriere dello Sport via Four Four Two)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anahofia mlinzi wake Joe Gomez,21 huenda akahitaji kufanyiwa upasuaji. (Liverpool Echo)

Newcastle wanajianda kutangaza kuondoka kwa kocha wao wa zamani Peter Beardsley ambaye alikua mkufunzi wa timu ya wachezaji wa chini ya miaka -23. (Mail)
Manchester United watampatia kazi meneja wao wa sasa Ole Gunnar Solskjaer akifanikiwa kushinda Paris St-Germain katika mchuano wao wa ligi ya mabingwa. (Sun)

Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino ameelezea kutoridhishwa kwake na usimamizi wa klabu hiyo baada ya kushindwa kusajili wachezaji wapya kwa misimu miwili mfululizo. (Mirror)

Chelsea watakabiliana na Bayern Munich katika uhamisho wa mshambuliaji Callum Hudson-Odoi, baada ya klabu hiyo ya Bundesliga kushindwa kumsajili nyota huyo wa miaka. (Sun)

Winga Willian, 30 wa Chelsea na Brazil, anataka kusaini mkataba wa miaka mitatu, lakini kuna tetesi amepewa mkataba wa mwaka mmoja. (Sport Witness)

Meneja wa West Ham Manuel Pellegrini alitaka kumsaini mchezaji wa zamani wa Cardiff, Gary Medel mwezi Januari lakini juhudi zake zilitibuka baada ya Besiktas kuitisha ada ya uhamisho. (Talksport)

Solskjaer: Pogba anafaa kuwa nahodha wa Man Utd
Meneja wa Inter Milan Luciano Spalletti anaamini Arsenal "walimlaghai" winga wa Croatia Ivan Perisic, 29, katika pendekezo la uhamisho wa Januari. (Rai Sport via Independent)
chanzo; bbc swahili
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz