SIMBA AUNGURUMA NYIKANI HUKU AKIMLIZA KARIOBANG SHARKS - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Monday, 4 June 2018

SIMBA AUNGURUMA NYIKANI HUKU AKIMLIZA KARIOBANG SHARKS

Wachezaji wa Simba SC

Kikosi cha Simba kimefanikiwa kusonga mbele mpaka hatua ya nusu fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup kwa ushindi wa matuta 3-2 dhidi ya Kariobang Sharks ya Kenya.

Mchezo uliokuwa uanpigwa Uwanja wa Afraha, umeshuhudiwa ukimalizika ndani ya dakika 90 huku kila timu ikishindwa kuona lango la timu pinzani.

Baada ya dakika 90 kumalizika hatua ya upigaji wa matuta ulifuatia na Simba ikaweza kupata penati mbili zilizofungwa na Erasto Nyoni, Haruna Niyonzima na Jonas Mkude.

Matokeo hayo yanaifanya Simba kuwa timu ya kwanza kuingia nusu fainali baada ya Yanga na JKU zote kutolewa jana.

Baada ya Simba kuvuka robo fainali leo, Tanzania itawakilishwa tena na Singida United kesho katika Uwanja huohuo wa Afraha.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ