KAULI TATA YA MANJI KUELEKEA MKUTANO MKUU WA YANGA - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Friday, 8 June 2018

KAULI TATA YA MANJI KUELEKEA MKUTANO MKUU WA YANGA


Kuelekea mkutano mkuu wa yanga wanachama,mashabiki na viongozi wanaonekana kuwa na wazo la mabadiliko kwenye klabu yao kutokana na hali ya klabu kwa sasa jinsi ilivyo.

Viongozi wengi wameachia ngazi zao kabla ya mkutano huo.

kumekuwepo na taarifa ya kwamba huenda Mwenyekiti aliejiudhuru wa klabu hiyo Yusuph manji akarudi kwenye timu hiyo kwa mara nyingine.

Kuelekea mkutano huo Yusuph maji ametoa kauli tata kama atahitajika kurudi kwenye klabu hiyo.

Yusuph manji alisema "Yanga ni klabu yetu sote na binafsi hii ni kama sehemu ya familia yangu. Kuona klabu inasuasua kiasi hiki sifurahi, wapo waliotufikisha hapana lazima wawajibike kwa mizani ya uongozi bora ili sote tuungane kuijenga upya klabu katika misingi bora na endelevu.
 Misingi endelevu ili yeyote yule mwenye mapenzi mema na klabu weledi katika uongozi aweze kuiongoza ,binafsi sona pingamizi kurejea endapo watawajibika waliotuvuruga, wanachama kuridhia kuijenga yanga upya yenye mtazamo chanya wa kimaendeleo pamoja na miundo mbinu"

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ