SIMBA NI NOOMA!!!!YAJA HII TENA - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Tuesday, 5 June 2018

SIMBA NI NOOMA!!!!YAJA HII TENA

SIMBA


Simba Sports Club imekuwa mbele katika kuanzisha vitu vipya kwa kukuza ufanisi na morali za wachezaji wake.
Ikumbukwe kuwa Simba SC ndiyo ilikuwa ya kwanza kuwa na tunzo za wachezaji wake kila mechi na kila mwezi.

Mo Simba Award zimeanzishwa na Mwekezaji katika klabu ya Simba SC, Mohammed Dewji kwa lengo la kutoa zawadi kwa wanafamilia wa Simba ambao wamesaidia klabu kupata mafanikio kwa msimu wa 2017/2018.

Tuzo hizi zitakuwa na vipengele 17 ambavyo vitahusisha wachezaji, benchi la ufundi, viongozi, mashabiki na wasimamizi wa mchakato wa mabadiliko.

Sherehe za kuwakabidhi zawadi washindi zitafanyika mwezi huu wa Juni 2018.

Imetolewa na Idara ya Habari, Simba SC.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ