ZIFAHAMU TIMU ZITAKAZOWAKILISHA TANZANIA KWENYE KOMBE LA SPORTPESA - EDUSPORTSTZ

Latest

ZIFAHAMU TIMU ZITAKAZOWAKILISHA TANZANIA KWENYE KOMBE LA SPORTPESA


Timu nane zitashiriki mashindano ya kombe la Sport Pesa jijini Nairobi

Bingwa mtetezi Gor Mahia ni miongoni mwa timu nane za Kenya na Tanzania zitakazoshiriki mashindano ya kombe la SportPesa Super Cup mwezi wa sita mjini Nairobi.

Jumla ya dola 57,500 zitashindaniwa katika mashindano hayo ya wiki moja yatakayofanyika katika uwanja wa Kasarani...John Nene anaangazia mashindano hayo.

Gor Mahia ni miongoni mwa timu nne za Kenya zitakazoshiriki pamoja na watani wao wa jadi AFC Leopards, Kariobangi Sharks na Kakamega Homeboyz.

Wawakilishi wa Tanzania ni bingwa wa ligi kuu Simba,Yangs Singida FC na Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) ya Zanzibar.

Afisa mkuu wa mauzo ya kampuni ya mchezo wa kubahatisha SportPesa, Kelvin Twissa, anasema mashindano haya yatazidi kuboresha uhusiano mzuri kati ya Tanzania na Kenya.

``Tumechagua timu bora zilizonawiri katika ligi zao kuu za nyumbani mwaka jana, na pia hii ni njia moja ya kukuuza vipaji vya kandanda eneo letu,'' alisema Twissa.

Mshindi wa mashindano hayo atasafiri hadi England kutoana jasho na Everton katika uwanja wao wa Goodison Park mwezi wa saba.


Bingwa mtetezi Gor Mahia ndiyo iliyocheza na Everton mwaka jana jijini Dar es Salaam ikapoteza kwa mabao 2-1, wafungaji wa Everton wakiwa ni mchezaji nyota wa zamani wa Manchester United Wayne Rooney na Kieran Dowell, naye Jacques Tuyisenge akaipa Gor Mahia bao lao moja.

Gor Mahia ilifuzu kucheza na Everton ilipoibuka mshindi wa mashindano ya SportPesa Super Cup kwa kuizaba AFC Leopards mabao 3-0 mechi ya fainali jijini Dar es Salaam.

Katika mechi za robo-fainali, AFC Leopards ilishinda Singida FC kwa mabao 5-4 ya penalti baada ya sare ya bao 1-1, Yanga ikashinda Tusker ya Kenya mabao 4-2 ya penalti kutokana na sare tasa, Gor Mahia ikainyoa Jang'ombe 2-0 na Simba ikakatwa mkia na Nakuru All Stars ya Kenya kwa kumeza mabao 5-4 ya penalti kutokana na sare tasa.

Matumaini ya Nakuru All Stars kusonga mbele yalifikia kikomo mechi za nusu fainali ilipolimwa mabao 2-0 na Gor Mahia, huku Leopards ikiing'oa Yanga kwa mabao 4-2 ya penalti baada ya sare ya kutofungana. Katika mechi ya fainali Gor Mahia ilizima kidomodomo cha Leopards kwa mabao 3-0.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz