Type something and hit enter

By OnUfaransa inatarajia kuweka sheria maalum ya umri wa kuanza kufanya mapenzi kuwa ni miaka 15. Hivyo
kufuatia mapendekezo hayo mtu yeyote atakayebainika kufanya mapenzi chini ya umri huo atakuwa amebaka.

Maamuzi haya yamekuja nchini humo mara baada ya madaktari na wanasheria kutoa ushauri wao kuhusiana na umri mtu anaostahili kuanza kufanya mapenzi.

Mabadiliko haya yamekuja kufuatia kesi mbili za hivi karibuni nchini Ufaransa zilizohusisha wanaume waliofanya mapenzi na wasichana waliokuwa na umri wa miaka 11.

Katika sheria ya sasa, kama mtu amekutwa na kosa la kufanya mapenzi na mtu chini ya miaka 15 iwe kwa hiari ama makubaliano, mshtakiwa atahukumiwa kwa kosa la kujamiana na mtoto lakini sio kosa la ubakaji.

Kosa hilo litamlazimu mshtakiwa kutoa kiasi cha dola 87,000 kama sehemu ya adhabu na kwenda jela miaka mitano.

Hukumu ni sawa kwa wanaofanya unyanyasaji kwa watu wazima na watoto lakini kosa la ubakaji huwa lina adhabu kubwa zaidi.Rais Emmanuel Macron

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron anaunga mkono mpango huo wa kuweka kiwango cha umri wa kuanza kufanya mapenzi.

Mwishoni mwa mwaka jana, mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 30 alikutwa hana hatia baada ya ushahidi kueleza kuwa aliyefanyiwa vitendo hivyo hakuwa amelazimishwa wala kupewa vitisho vyovyote.

Hata hivyo wakati msimamo huo ukitolewa huko nchini Ufaransa hali ni tofauti katika maeneo mengine barani Ulaya. Sheria ya kujihusha na mapenzi inaruhusu katika umri tofauti;
Ulaya

Austria,Ujerumani,Italia ni miaka 14

Ugiriki, Poland, Sweden ni miaka 15

Ubeligiji, Netherland, Spain, Urusi na Uingereza ni miaka 16


Umri wa kuanza kufanya mapenzi Afrika


12

Angola (Taifa lenye umri mdogo zaidi)


14 Botswana (wanaume), Cape Verde, Chad (wasichana), DRC (wasichana), Lesotho (wanaume), Madagascar na Malawi


20 Tunisia (Taifa lenye umri mkubwa zaidi)

BBC
Barani Afrika

Miaka 12; Angola

Miaka 13; Burkina Faso, Comoro, Niger

Miaka 14; Botswana (wanaume), Cape Verde, Chad (wasichana), Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (wasichana), Lesotho (wanaume), Madagascar na Malawi

Miaka 15; Guinea, Morocco

Miaka 16; Algeria, Botswana (wanawake), Cameroon, Ghana, Guinea Bissau, Lesotho (wanawake), Mauritania, Mauritius, Mozambique, Namibia, Senegal, Afrika kusini, Swaziland, Togo, Zambia, Zimbabwe.

Miaka 18; Benin, Burundi, Afrika ya kati,Ivory Coast, DRC (wanaume), Djibouti, Equatorial Guinea, Eritrea, Ethiopia, Gabon, Gambia, Kenya, Liberia, Mali, Nigeria, Republic of Congo, Rwanda, Seychelles, Sierra Leone, Somalia, South Sudan, Tanzania, Uganda.

Miaka 20; Tunisia

Wakati ukatili wa kimapenzi kwa watoto ni kosa la jinai katika nchi nyingi za Afrika bado katiba za nchi hizo zimetoa mwaya kutokana na mila na desturi na kupelekea kuendelea kuwepo kwa mimba za utotoni na ndoa za utotoni.

Kwa mfano nchini Tanzania, ni hatia kwa mtu kujihusisha na mapenzi chini ya umri wa miaka 18 na kutajwa kuwa ni unyanyasaji kwa watoto na kinyume cha sheria.

Huku kuna mkanganyiko ambapo kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya mwaka 1971 inaruhusiwa mtu kufunga ndoa akwa na umri wa miaka 14.Ukatili wa kimapenzi kwa watoto ni kosa la jinai katika nchi nyingi za Afrika

Nchini Kenya umri sahihi wa kuanza kujihusisha na mapenzi ni miaka 18 na yeyote aliye chini ya umri huo anatambuliwa kuwa ni mtoto. Ingawa ndoa pia inawezekana kufungwa katika umri huo, sheria haijaweka wazi.

Katika vigezo hivyo vya umri, Angola ikiwa ni nchi pekee ya barani Afrika iliyoweka umri mdogo zaidi ya watu kujihusisha na ngono, wa miaka 12.

Mara nyingi nchi nyingi barani Afrika huwa hawaweki wazi suala hili la umri wa kuanza kujihusisha na mapenzi kutokana na mila na desturi pamoja na imani za dini.

Na kwa upande wa Umoja wa mataifa hakuna sheria au muongozo maalum kuhusu umri ambao unaruhusu mtu kuanza kufanya tendo hilo, licha ywa kwamba kuna haki za kumlinda mtoto.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ
Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Click to comment