TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA LEO 18.05.2018 - EDUSPORTSTZ

Latest

TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA LEO 18.05.2018

Mikel Arteta

Kiungo wa kati wa zamani wa Arsenal Mikel Arteta, 36, anakaribia kuchukua mahala pake Arsene Wenger huko Emirates. (Daily Telegraph)

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola na mkurugenzi wa kandanda Txiki Begiristain wamempa ruhusa naibu kocha Arteta kuzungumza na klabu yake ya zamani. (Sport)
Rafael Benitez
Arsenal pia wana nia ya kuzungumza na Thierry Henry kuhusu nafasi ya umeneja iliyo wazi mapema wiki ijayo. (Sky Sports)

Rafael Benitez, anayeaminiwa kutafutwa na West Ham atachagua kubaki kama maneja wa Newcastle lakani anataka kuhakikishiwa kuhusu bajeti ya kununua wachezaji kutoka mmiliki wa klabu Mike Ashley. (Daily Telegraph)

Gianluigi Buffon
Benitez anataka pauni milioni 100 za kununua wachezaji kuwa mwamuzi mkuu kuhusu kuwanunua wachezaji na mshahara wa pauni milioni 6 kwa mwaka ili kuweza kusalia huko St James' Park. (Daily Express)

Liverpool wanataka kipa raia wa Italia Gianluigi Buffon, 40, ambaye amaendoka Juventus baada ya miaka 17, lakini huenda wakakabiliwa na ushindani kutoka Manchester City. (Sun)

Alvaro Morata
Juventus wanataka kurudisha Alvaro Morata ambaye alichezea klabu hiyo kati ya mwaka 2014 na 2016. Mchezaji huyo wa miaka 25 alifunga magoli 11 katika mechi 31 za Premier League wakati wa msimu wake wa kwanza huko Chelsea. (Independent)

Chelsea wamekana kuamruhusu mchezaji wa mkopo Michy Batshuayi, 24, kujiunga na Borussia Dotmund, lakini wanakaribisha klabu hiyo ya Ujerumani kumsaini Morata. (Daily Mirror)

Sergio Aguero
Mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero, 29, anasema anatarajia tu kucheza na nyota wa Barcelona Lionel Messi katika kikosi cha Argentina, anasema ama afura kuwa huko Etihad. (Corriere dello Sport in Italian)

Ajenti wa kiungo wa safu ya kati wa Napoli Jorginho anasema mchezaji huyo atahamia Manchester City ikiwa vilabu hivyo vitakubaliana kuhusu fedha. Napoli wanataka hadi pauni milioni 60 kwa mchezaji huyo wa miaka 26 lakini City wanataka wakubaliane kiwango kinachokaribia pauni milioni 50. (Manchester Evening News)

Kalidou Koulibaly

Napoli wametangaza euro milioni 120 kwa mchezaji wa kimataifa raia wa senegal Kalidou Koulibaly, 26, katika jaribio la kuzuia Real Madrid, Chelsea na Manchester United. (RAI Sport, via Football Italia)
Shakhtar Donetsk wametangaza kuwa kocha mkuu Paulo Fonseca - ambaye amehusishwa na West Ham na Everton amesaini mkataba wa miaka miwili. (Shakhtar Donetsk)

Leicester wamekubaliana pauni milioni 17.5 na Porto kwa mlinzi Ricardo Pereira, 24. (A Bola, via Leicester Mercury)

Klabu iliyoshindwa ya West Brom inatarajiwa kumtafuta meneja mpya wiki hii na inaweza kumgeukia kocha mkuu wa Brentford Dean Smith, 47. (London Evening Standard)

Mshambulizi wa Paris St-Germain Mbrazil Neymar, 26, amerejea mazoezi baada ya kupata jeraha mwezi Februari (Daily Mail)
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz