TAMBO ZA RAYON SPORTS ZAISHIA KUTOA SULUHU NA YANGA UWANJA WA TAIFA - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Wednesday, 16 May 2018

TAMBO ZA RAYON SPORTS ZAISHIA KUTOA SULUHU NA YANGA UWANJA WA TAIFA
KIKOSI CHA RAYON SPORTSDakika 90 za mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Yanga dhidi ya Rayon Sports kutoka Rwanda zimemalizika katika Uwanja wa taifa, Dar es Salaam kwa matokeo ya suluhu ya 0-0.

Mchezo huo ulionekana kwa kila timu kucheza kwa uangalifu zaidi huku wote wakikosa nafasi kadhaa za kufunga ikiwemo Yanga kupitia Chirwa aliyegongesha mwamba mnamo kipindi cha pili.

Mchezo ambao ni wa pili kwa timu zote mbili katika hatua ya makundi ya michuano hiyo unaiweka Yanga katika mazingira magumu ambapo mpaka sasa inakuwa imeambulia pointi moja pekee.

Ikumbukwe katika mechi iliyopita Yanga ilikubali kupoteza kwa jumla ya mabao 4-0 dhidi ya dhidi ya USM Alger huko Algiers, Algeria.

Wakati huo Rayon Sports inakuwa imejikusanyia alama 2 kwenye kundi hilo 'D' baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Gor Mahia FC ya Kenya kwenye mechi yake ya kwanza iliyopigwa Kigali, Rwanda.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ