MRITHI WA WENGER ARSENAL AFAHAMIKA - EDUSPORTSTZ

Latest

MRITHI WA WENGER ARSENAL AFAHAMIKA

  Unai Emery 

Emery anatarajiwa kupewa kazi ya kuwa meneja mpya wa Arsenal

Klabu ya Arsenal inatarajiwa wiki hii itamtangaza Unai Emery,kuwa meneja mpya wa klabu hiyo kuchukua mikoba ya Arsene Wenger.

Emery aliiacha na klabu yake ya Psg, mwanzoni mwa mwezi huu na alikuwa jijini London, jana jumatatu, kufanya mazungumzo na klabu ya Arsenal ya kuwa meneja mpya wa washika mitutu hao wa London.

Meneja huyu raia wa Hispania, mwenye umri wa miaka 46,aliisaidia klabu ya Psg, kutwaa mataji matatu katika msimu ulimalizika katikati ya mwezi huu na nafasi yake katika miamba hao wa Ufaransa imechukuliwa na Thomas Tuchel.

Kwa siku za karibuni kiungo wa zamani wa Arsenal Mikel Arteta ndio alitajwa angepewa jukumu la kupewa kazi ya umeneja ya kuwaongoza Arsenal baada ya miaka 22, ya kuongozwa na Arsene Wenger.Santi Cazorla anaondoka katika timu ya Arsenal

Wakati huo huo kiungo wa Arsenal Santi Cazorla anaondoka klabuni hapo msimu huu baada ya kumalizika kwa mkataba wake, Cazorla ameichezea timu yake jumla ya michezo 180 toka alipojiunga na klabu hiyo mwak 2012 akitokea Malaga.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz