FABINHO KUTUA LIVERPOOL - EDUSPORTSTZ

Latest

FABINHO KUTUA LIVERPOOL

Fabinho

Fabinho anatarajia kuchukua nafasi ya Emre Can ambaye anatimkia Juventus
Liverpool imekubali kumsajili kiungo wa Monaco Fábio Henrique Tavares maarufu kama Fabinho kwa ada ya Paundi Milioni 40 ambayo inaweza kuongezeka kutokana na kiwango cha mchezaji.

Fabinho mchezaji wa kimataifa wa Brazil mwenye miaka 24 atajiunga na Liverpool Julai 1.

Kiasi cha ziada cha ada ya uhamisho wake ambacho ni Paundi Milioni 5 kinaweza kuongezeka kutokana na mafanikio atayoipa Liverpool.

Kuwasili kwake ni kwa ajili pia ya kuziba pengo la Emre Can ambaye anatarajiwa kutimkia kwa mabingwa wa Seria A Juventus muda wowote.

Image caption
Fabinho alijiunga na Monaco akitokea Rio Ave ya Ureno mwaka 2013
''Hiki ni kitu ambacho sikuzote nimekuwa nikikitamani- hii ni timu kubwa, ''alisema Fabinho. ''Nimefurahishwa sana.''

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema ''Huyu ni mchezaji ambaye ana faida sana uwanjani, anaweza kucheza nafasi nyingi, namba sita, nane ama namba mbili'. Hili ni jambo zuri sana.''

Fabinho ambaye mkataba wake unatarajiwa kuanza Julai 1 amesema Liverpool ni klabu yenye miundombinu mizuri na ya kuvutia.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz