WACHEZAJI WA SIMBA WATAKAOIKOSA KAGERA SUGAR LEO - EDUSPORTSTZ

Latest

WACHEZAJI WA SIMBA WATAKAOIKOSA KAGERA SUGAR LEO

Wachezaji wa Simba

Kikosi cha Simba kinaingia Uwanja wa Taifa leo kucheza mchezo wa ligi dhidi ya Kagera Sugar FC katika mechi ambayo itakuwa ya kukabidhiwa ubingwa wake.

Mechi hiyo itahudhuriwa na mgeni rasmi ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli, ili kuwakabidhi Simba taji lao jipya la msimu wa 2017/18.

Simba itacheza mchezo huo bila kipa wake namba moja Aishi Manula pamoja na Yusuph Mlipili ambao watakuwa wanatumikia adhabu ya kuwa na kadi tatu za njano walizopata msimu huu tangu uanze.

Kukosekana kwa Manula leo kunatoa nafasi kwa makipa wa akiba kati ya Said Mohammed na James Mseja mmoja wao kucheza leo mbele ya Rais Magufuli.

Mechi hiyo itaanza majira ya saa 8 kamili mchana ili kuwapa nafasi waliofunga kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kuwahi futari majumbani.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:

Delivered by EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz