PAUL MAKONDA KUZUNGUMZA NA WANAHABARI LEO KUHUSU SIMBA - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Friday, 18 May 2018

PAUL MAKONDA KUZUNGUMZA NA WANAHABARI LEO KUHUSU SIMBA

Paul makonda
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh, Paul Makonda ameitisha kikako maalum na Wanahabari kikatachofanyika katika ofisi zake zilizopo Ilala Boma, Dar es Salaam kuzungumzia kile kitakachpfanyika kesho Uwanja wa Taifa.

Taarifa zinaeleza Mh. Paul Makonda atazungumzia machache kuhusiana na mechi ya Simba SC dhidi ya Kagera Sugar ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

Aidha, Makonda ataambatana na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Ndugu, Haji Manara katika kikao hicho.

Ikumbukwe Simba itakuwa ina kibarua kesho Jumamosi katika Uwanja wa Taifa kukipiga na Kagera Sugar, mechi itakayoenda sabambamba na wekundu hao wa Msimbazi kukabidhiwa taji lao jipya la Ligi Kuu Bara msimu huu na Mh. Rais Magufuli.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ