TAMKO LA ALIKIBA KUHUSU VIDEO YAKE MPYA KUFANYIWA FIGISU YOUTUBE - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Monday, 14 May 2018

TAMKO LA ALIKIBA KUHUSU VIDEO YAKE MPYA KUFANYIWA FIGISU YOUTUBE

Video ya wimbo wa ‘Mvumo wa Radi’ ya Msanii wa Bongo Fleva, Alikiba imeelezwa kuwa imefanyiwa figisu figisu hususani kwenye suala la Watazamaji (Views) kwa kile kilichoelezwa kuwa hawaongezeki toka itoke video hiyo siku ya Ijumaa.
Msanii wa Bongo Fleva, Alikiba.


Mvumo wa Radi  video mpya ya msanii mkongwe wa bongo fleva "Alikiba" ilitazamiwa kupokelewa kwa shangwe na wingi kwani watanzania wengi walikua wameingojea kwa kipindi kirefu tangu atoe wimbo wake wa SEDUCEME uliovunja rekodi ya kutazamwa na watu wengi ndani ya msaa 24. 


Mpokeo ya Wimbo huo umewashutua wengi kwani tangu kutoka kwake siku ya ijuuma ijafikisaha 1M viewers Kitu ambacho kimesemekana ni mchezo mchafu wa figisu uliochezwa ili kupunguza watazamaji wa wimbo huu.

Alikiba amesema amepokea malalamiko hayo na hata hao wenyewe wamelitambua tatizo hilo na tayari wametuma malalamiko hayo makao makuu ya YouTube Afrika kuweza kutatua changamoto hiyo, na kuwaomba mashabiki wake waendelee kutazama kichupa hicho.

“Tunafahamu tatizo la kutokuongezeka kwa views kwenye akaunti ya YouTube ya ALIKIBA, na tupo kwenye mawasiliano ya moja kwa moja na makao makuu ya YouTube Africa ambao wanafanya kila jitihada kutatua tatizo hili kwa haraka iwezekanavyo. Shukrani kwa uvumilivu wenu na support mnayoendelea kutupa! Endeleeni kuangalia video ya Mvumo wa Radi,“ameeleza Alikiba kwenye taarifa yake kwa umma.

Video ya Mvumo wa Radi tangu jana Mei 12, 2018 imekuwa namba moja kwenye Trending ya video zinazotazamwa zaidi Tanzania na mpaka sasa bado ipo namba moja lakini tangu jana licha ya kuwa namba moja bado views wanaongezeka taratibu sana ukilinganisha na siku ya Ijumaa.

Kwa siku ya Jana hadi jana usiku waliongezeka  watazamaji chini ya 70+k ile hali kwa siku ya Ijumaa hadi Jana Jumamosi video hiyo ilikuwa imetazamwa na watu 690+k .

Hii sio mara ya kwanza kwa msanii wa Bongo Fleva kuhusu figisu figisu za views kwenye mtandao wa YouTube kwani Baraka The Prince alishawahi kukiri kuwa kuna watu wanamfanyia mchezo huo.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ