WENGER APOKEA ZAWADI KUTOKA KWA SIR ALEX FERGUSON - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Monday, 30 April 2018

WENGER APOKEA ZAWADI KUTOKA KWA SIR ALEX FERGUSON

  

Kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson leo amemuaga kocha wa Arsenal Arsene Wenger kwa kumpa zawadi maalum kabla ya mechi ya ligi kuu iliyomalizika kwa kufungwa 2-1 usiku huu kuanza.

Fergusona amemkabidhi zawadi hiyo kwaniaba ya klabu ya Manchester United ikiwa ni sehemu ya kutambua mambo mbalimbali ambayo Wenger ameyafanya kwenye ligi kuu ya soka ya England EPL.

Wenger ametangaza rasmi kuachana na Arsenal aliyoifundisha kwa miaka 22 mwishoni mwa msimu huu. Hata hivyo Wenger bado hajaweka wazi kama atastaafu au atakwenda kufundisha timu nyingine.

Katika mchezo uliopigwa jioni hii kwenye uwanja wa Old Trafford, Wenger ameshinwa kulinda heshima ya kutofunga baada ya vijana wake kuruhusu bao la dakika za mwisho kutoka kwa Marouane Fellaini.

Mabao ya Man United yamefungwa dakika ya 16 na kiungo Paul Pogba na dakika ya 90 na Marouane Fellaini huku lile la Arsenal likifungwa na Henrikh Mikhtaryan dakika ya 51. Wenger na Mourinho sasa wamekutana mara 13 na Mourinho ameshinda mara 8 na kutoka sare mara 5.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

No comments:

Post a Comment