UJUMBE WA TFF KWA YANGA KUELEKEA MECHI YAKE DHIDI YA DICHA - EDUSPORTSTZ

Latest

UJUMBE WA TFF KWA YANGA KUELEKEA MECHI YAKE DHIDI YA DICHA
Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF limesema kuwa imani yao kwa Yanga ni kubwa na wanaamini timu hiyo itaibuka na matokeo mazuri kwenye mchezo wa marudiano kesho dhidi ya Welayta Dicha


Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Salum Madadi, amebainisha hayo leo, ambapo amesema Yanga inaweza kuitoa Woilata Dicha, kama watatumia tena udhaifu ulioonekana kwa wapinzani hao, kwenye mchezo wa kwanza.

''Yanga ni timu bora na walionesha hilo kwenye mchezo wa kwanza kwa kuwafunga Dicha mabao 2-0 kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam hivyo tuna imani kubwa sisi kama shirikisho Yanga watalinda ushindi wao na kusonga mbele hatua ya makundi'', amesema.

Madadi ameongeza kuwa kocha wa Yanga aliyeondoka George Lwandamina amepata CV nzuri akiwa na klabu hiyo, kwa hiyo si jambo geni kwa makocha wa nje kuondoka pale wanapopata mafanikio Tanzania.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:

Delivered by EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz