MAN CITY VINARA WA CLUB BINGWA EPL - EDUSPORTSTZ

Latest

MAN CITY VINARA WA CLUB BINGWA EPL

EDUSPORTSTZ inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

Jana April 15 2018 game ya Man United dhidi ya West Bromwich Albion imethibitisha rasmi kuwa club ya Man City ndio Bingwa wa EPL msimu 2017/2018, hiyo ni baada ya Man United aliyekuwa nafasi ya pili kupoteza mchezo dhidi ya Wets Bromwich leo kwa goli 1-0.

Man City wametangazwa kuchukua taji la EPL kwa mara ya tano baada ya wapinzani wao wakuu waliyokuwa wanawafuatia nafasi ya pili Man United kupoteza wakiwa nyumbani, hivyo Man City wametangazwa kuwa Mabingwa kwa kuwa na jumla ya point 87 na wamesalia na michezo mitano, Man City mara ya mwisho kutwaa taji la EPL ilikuwa mwaka 2014.

Hivyo Man City ambao wao wamecheza game yao ya EPL wiki hii Jumamosi ya April 14 dhidi ya Tottenham na kushinda magoli 3-1, wanatangazwa Mabingwa kwani hata Man United akishinda game zake zote na Man City akapoteza game zote zilizosalia, Man United atakuwa na point 86 hivyo hakuna club ya EPL inayoweza kufikia point za Man City 87.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz