THAMANI YA MSUVU KUPANDA KUFIKIA BIL 1.3 "MSUVA" AFUNGUKA HAYA - EDUSPORTSTZ

Latest

THAMANI YA MSUVU KUPANDA KUFIKIA BIL 1.3 "MSUVA" AFUNGUKA HAYA

Kiungo mshambuliji wa timu ya Diffaa Al Jadi­da ya nchini Morocco, Simon Msuva (katikati).

SIMON Msuva ni kiungo mshambuliji wa timu ya Diffaa Al Jadi­da ya nchini Morocco ambaye ametua katika klabu hiyo mwanzoni mwa msimu huu akitokea Yanga.

Msuva ni miongoni mwa wachezaji wachache wa Kitanzania wanaowakilisha nchi nje ya nchi wakicheza soka la kulipwa ambapo ameonyesha uwezo wa hali ya juu katika katika klabu yake hiyo kutokana na ubora wake katika kuzoea mazin­gira mapema na kuwa mfungaji mzuri.

Alijiunga na Al Jadida, Julai 29, mwaka jana kwa dau la dola 150,000 ambalo ni zaidi Sh milioni 337 akitokea Yanga la­kini kwa sasa Waarabu wamemthamin­isha kwa euro 475,000, sawa na zaidi ya Sh bilioni 1.3.



Moja ya mikakati yake ni kuona anafanikiwa kusonga mbele zaidi ili aweze kumfikia Mtanzania mwen­zake, Mbwana Samatta anayekipiga katika Klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji.

Championi Ijumaa imefanya mazun­gumzo na kiungo huyo ambaye ameelezea mikakati yake pamoja na kupanda kwa tha­mani yake kwa sasa.

Mazungumzo hayo ilikuwa ni baada ya mchezo wa Taifa Stars dhidi ya DR Congo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar ambapo Msuva alipata nafasi ya kucheza na kuonye­sha uwezo mzuri.



UNAZUNGUMZIAJE MCHEZO DHIDI YA DRC?

“Tunashukuru Mungu kwa matokeo tuliyoya­pata, tumepoteza mchezo wetu dhidi ya Alge­ria lakini kuna kitu fulani tumejifunza kutoka kwao, tukicheza mechi nyingi inatusaidia ku­tuweka vizuri.



“DRC Congo wana timu nzuri ukiangalia mchezaji mmoja mmoja ni tofauti na tulivyo sisi lakini katika mpira lolote linaweza kuto­kea.

“Mpira unachezeka uwanjani na matokeo yanapatikana uwanjani, tulihamasishana wenyewe kwa wenyewe tuweze kuonyesha kitu na kweli tumefanikiwa kuonyesha kile ambacho Watanzania wanakihitaji.

“Tuliingia uwanjani kama timu, ma­kocha walituhamasisha, manahodha pamoja na wachezaji kwa ujumla tu­lijipanga ili kuhakikisha tunafanikiwa kufanya vyema na kweli matunda yam­eonekana kwa kupata ushindi.

UNAZUNGUMZIAJE SAPOTI YA MASHABIKI?

“Naomba mashabiki waiamini timu yao, shabiki kazi yake ni kushangilia timu yake, watambue kwamba timu ni hiihii hakuna tofauti, naamini tutafanya vizuri, waendelee kutupa sapoti ili tu­fanye vyema, wenzetu nje mashabiki wanashangilia timu yao hata wakifun­gwa.

KUCHEZA LIGI YA MABINGWA UKIWA NA TIMU YA MOROCCO, INA MAANA GANI KWAKO?

“Ni furaha kwangu, ni mara yangu ya kwanza kucheza mashindano hayo ni­kiwa Morocco, ninafanya kazi na timu yangu kwa kushirikina na wenzangu, nahitaji kupita njia ya Samatta ili nipate mafanikio makubwa.

UNA MABAO MANGAPI HADI SASA?

“Katika Ligi ya Mabingwa nina mabao manne katika Ligi Kuu ya Morocco nina sita, siyo mwendo mbaya kwangu.

MOROCCO WANAMCHUKULIAJE MSUVA?

“Wamenieleza kuwa mimi ndiyo Mtanzania wa kwanza kuonyesha kiwango kizuri kama changu katika ligi yao, nimefika na kuonyesha mabadiliko ya haraka ndani ya muda mfupi, wananikubali sana. Nimekopi vitu vyao mapema kutokana na kujitambua.

KIPI KILIKUFANYA UZOEE MAPEMA?

“Ligi yao haina tofauti sana na ligi ya Bongo kikubwa ni ushindani tu, niweweza kukutana na watu wanaojua mpira na ndiyo maana nimebadilika kwa haraka, mwalimu ameni­tengeneza na kunibadilisha, nimekuwa na uwezo mzuri wa kucheza katikati na hata mechi ya Stars na Congo nimecheza kati.

UNAZUNGUMZIAJE KUPANDA THA­MANI YAKO?

“(Kumbuka thamani yake ya dau la usajili im­epanda na sasa ni Sh bilioni 1.3) Namshukuru Mungu kuona thamani yangu inaendelea kupanda siku hadi siku, kikubwa ninamshuku­ru Mungu na kila kitu kinawezekana kupitia yeye, nitaendelea kupambana ili nisonge mbele.”


EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz