ALIYOFUNGUKA KOCHA WA UFARANSA KUHUSU POGBA - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Tuesday, 20 March 2018

ALIYOFUNGUKA KOCHA WA UFARANSA KUHUSU POGBA

Paul Pogba

Kocha mkuu wa kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa Didier Deschamps amesema kwa sasa mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Paul Pogba hana furaha

Mshambuliaji huyo amekuwa si mtu mwenye furaha na kuonekana hapendwi katika uwanja wao wa Old Trafford.

Pogba yupo katika kikosi cha Ufaransa kwa ajili ya michezo ya kirafiki dhidi ya Colombia na Urusi alionekana kutopendezwa kwa kufanyiwa madadiliko na timu yake ya Manchester United katika mchezo wa jumamosi dhidi ya Brighton .

Didier amesema mengi atayasikia kuhusu hilo kwa Pogba ni hali ambayo haifai, United watakuwa na mchezo mwingine wa ligi kuu dhidi ya Swansea tarehe 31 Machi.

United itarudi katika mechi za ligi ya Uingreza dhidi ya Swansea mnamo tarehe 31 Machi.

Pogba alianzishwa katika kikosi cha United dhidi ya sevilla katika mechi ya vilabu bingwa Jumanne iliopita baada ya kukosa kushirikishwa katika mechi ya ushindi dhidi ya Liverpool kutokana na tataizo la jeraha.
Kocha wa Ufaransa Didier Deschamps

''Sijui kwa nini iwe hivyo, aliongezea Deschamps. Ni kwa nini mambo yalifikia kiwango hicho, lazima kuna sababu''.

''Mimi huzungumza sana na wachezaji katika kambi ya mazoezi ili kujua hisia zao . Sio Pogba pekee''.

Pogba alijiunga na United mwaka 2016 kwa ada ya pauni milioni 89 na mpaka sasa ameisaidia United kushinda Kombe la ligi na Europa League msimu uliopita.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ