BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Thursday, 15 February 2018

TETESI ZA SOKA LA ULAYA LEO ALHAMISI TAREHE 15.2.2018
Tottenham wana nia ya kumpa meneja Mauricio Pochettino mkataba mpya wa pesa nyingi. Raia huyo wa Argentina aliweka sahihi mkataba mpa ya miaka mitano mwaka 2016 wa pauni milioni 5.5 kwa mwaka. (Telegraph)

Real Madrid wanaongoza mbio za kumwinda mlinzi wa Tottenham Toby Alderweireld. Manchester City, Chelsea na Manchester United pia nao wanamwinda mbelgiji huyo wa miaka 28. (Mirror)=

Kiungo wa kati wa Manchester United Marouane Fellaini amekubali kujiunga na Besiktas mwisho wa msimu. Mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji, 30, utakamilika mwisho wa msimu. (Fotomac - in Turkish)

Jeventus wameuliza kuhusu kiungo wa kati wa Liverpool Jack Wilshere ambaye mkataba wake unakamilika msimu huu. (Mirror)

Everton na Tottenham wote wanamzea mate wing'a wa PSV Steven Bergwijn. Mchezaji huyo wa miaka 20 aliiwakilisha uholanzi katika kwenye kikosi cha chini ya miaka 17 na 21. (ESPN)

Kiungo wa kati wa Tottenham Erik Lamela anaeleza kuhama kwake kwenda Inter Milan. Muargentina huyo amerejea tu baada ya jeraha lililomweka nje kwa zaidi ya mwaka mmoja. (Talksport)

Arsenal na Chelsea wote wanafuatilia mkataba wa mlinzi Luke Shaw wa Manchester United. Jose Mourinho amethibitisha kuwa mlinzi huyo yuko katika mkondo wa mkataba mpya lakini mazungumzo bado hayajaanza. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Manchester United raia wa Ufaransa Paul Pogba, 24, anataka meneja Jose Mourinho kubadili mfumo ya kikosi ili apate kushiriki katika safu ya mshambuliaji (Daily Record)

Meneja wa Stoke Paul Lambert anasema kuwa kipa Jack Butland, 24, hataathiriwa na uvumi kuhusu hatma yake (Stoke Sentinel)

Mshambuliaji wa Manchester City Gabriel Jesus, 20, ametafuta usaidizi wa mBrazil mwenzake baada ya kuchukua muda mrefu kupona jeraha. Wote hao walikutana katika sherehe ya siku ya kuzaliwa ya Neymar wiki iliyopita. (Daily Mail)

Everton wamemsadia shabiki wa miaka 100 kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kumualika kwenye mazoezi yao pamoja na kikombe cha chai na mshambuliaji wa zamani wa Everton Duncan Ferguson. (Liverpool Echo)
Elimu Yetu
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ

1 comment:

  1. Tafadhali: Jack Wilshere ni mchezaji wa Arsenal na siyo Liverpool

    ReplyDelete