TENGA ACHUKUA NAFASI YA MALINZI BMT - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Friday, 9 February 2018

TENGA ACHUKUA NAFASI YA MALINZI BMT


Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amemteua Leodgar Tenga (pichani) kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Dionis Malinzi kabla ya uteuzi wake kutenguliwa mwezi Julai mwaka jana.

Waziri Mwakyembe pia amewateua wajumbe sita wapya kuunda baraza hilo.

Wajumbe hao ni pamoja na: Prof. Mkumbwa Mtambo, Beatrice Singano, Kanali Mstaafu Juma Ikangaa, John Joseph Ndumbaro, Rehema Sefu Madenge na Salmin Kaniki.

Wengine wanaoingia kutokana na nafasi zao ni pamoja na Yusuph Singo ambaye ni mkurungenzi wa maendeleo ya michezo kutoka katika wizara hiyo, Dkt. Edicome Shirima ambaye ni kamishna wa elimu kutoka wizara ya elimu pamoja na Katibu Mkuu wa Baraza hilo ambaye ni Mohamed Kiganja.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kitengo cha mawasiliano cha baraza hilo, uteuzi huo umeanza rasmi jana, Februari 8, 2018 ambapo wote walioteuliwa watalitumikia baraza hilo kwa kipindi miaka miatatu.

Uteuzi huo unafanyika ikiwa ni takriban miezi nane imepita tangu waziri huyo alivunje baraza lililokuwepo awali chini ya uenyekiti wa Dionis Malinzi mwezi Julai mwaka jana kutokana na kutoridhika na utendaji wake.

Katika hatua nyingine Dkt. Mwakyembe amemteua Timothy Mganga kuwa Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya kwa kipindi cha miaka mitano. @edusportstznews


Elimu Yetu

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno.
Edusportstz

↑ Grab this Headline Animator

No comments:

Post a Comment