SABABU ZA GUARDIOLA KUGOMEA MKATABA MPYA MAN CITY - EDUSPORTSTZ

Latest

SABABU ZA GUARDIOLA KUGOMEA MKATABA MPYA MAN CITYMeneja wa Manchester City, Pep Guardiola amegoma kuingia kandarasi mpya mpaka pale atakapo hakikisha anaipatia taji timu hiyo.

Guardiola ambaye alikuwa kocha wa Barcelona amekubali kandarasi mpya aliyopewa na City itakayo mfanya kusalia katika viunga vya Etihad mpaka mwaka 2021 lakini kwa upande wake amenuwia kutomwaga wino hadi atakapo iwezesha timu hiyo kunyakuwa taji.

Mkataba huo wenye thamani ya pauni milioni 20 kwa mwaka utamfanya kocha huyo kuendelea kukinoa kikosi cha City ilhali ule wa sasa ukitarajiwa kufikia tamati mwishoni mwa msimu.

Mhispania huyo hakuwa na uhakika kama angekuwa zaidi ya miaka mitatu lakini hatimaye anasalia na kuendeleza ‘project’ yake City.

Habari kutoka ndani ya klabu hiyo zimesema kuwa, Guardiola anachohitaji ni kuhakikisha anatwaa taji lake la kwanza hapa kabla ya kusaini mkataba mpya na klabu.

Kikosi cha City kitakuwa na kazi kubwa wiki ijayo pale iatakapo kutana na Arsenal siku ya Jumapili katika kupigania taji la Carabao Cup katika dimba la Wembley.

Mmiliki wa klabu hiyo, Sheikh Mansour hana wasiwasi na Guardiola baada ya kukionyeshea dira kikosi cha timu hiyo huku ikiongoza ligi hiyo kwa wastani mzuri.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.

Delivered by EDUSPORTSTZ


Subscribe to EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz