ROONEY AFUNGUKA JUU YA UJIO WA SANCHEZ NA KUONDOKA KWA MKHITARYAN NDANI YA MAN UNITED - EDUSPORTSTZ

Latest

ROONEY AFUNGUKA JUU YA UJIO WA SANCHEZ NA KUONDOKA KWA MKHITARYAN NDANI YA MAN UNITED

Image result for rooney

Mchezaji wa timu ya taifa ya England na club ya Everton Wayne Rooney Amefunguka na kusisitiza sababu zilizomfanya Mourinho kumuuza Mkhitaryan na kuwasili kwa Alexis Sanchez

Wayne Rooney amesema kuma jose mourinhyo hakuwahi kumpa Henrikh Mkhitaryan nafasi ya kutosha kuonesha uwezo wake ndani ya Manchester United ndiyo maana hakuwahi kuona umuhimu wake.

Mkhitaryan aliwahi kuanza mara 26 katika mechi za epl akiwa ndni ya Manchester united katika kipindi cha miezi 18 aliyokaa katika clabu hiyo kabla ya kudakwa naArsenal mwezi uliopita.

Akizungumza juu ya Soka ya Jumatatu Usiku, Rooney alisema: "Nimewahi kumuona katika mazoezi mara kibao , ila kiukweli ni mchezaji mwenye kipaji cha hali ya juu".

"Nadhani huko Manchester United hakuwa na uhuru alioutaka ili kuonesha kipaji chake kama alivyokuwa na Dortmund na aina ya mchezo wa Dortmund pia inaweza kuwa sababu kubwa.

"Na katika Arsenal atawateka wachezaji kisoka,atachukua mpira na kufanya majabu. Kwa kweli nadhani atakuja kuwa tishio. "

Rooney pia alizungumza juu ya kuwasili kwa Alexis Sanchez huko United ubadilishaji wa Mkhitaryan na the Gunners na kusema;

"Kwa mimi yeye ni mchezaji sahihi kwa Manchester United, ana shida, shauku na tamaa ya kufanya makubwa kwani yeye pia ni mshindi kati ya washindi.

"Hiyo ndivyo ambavyo Manchester United ilikuwa ikiitaji kwa muda mrefu- wachezaji kama(Romelu),Lukaku ambao watamshika na kumsaidia kufunga mabao mengi zaidi.

"Wao ni wachezaji wa muhimu sana, karibu kama ilivyo kuwa kwa (Carlos) Tevez wakati alijiunga na United.

"Wachezaji kama hao kazi yao inakuwa ni wengine," aliongeza juu ya mtazamo wake kuhusu ujio wa sanchez ndani ya Manchester united EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz