MSUVA HAKAMATIKI - EDUSPORTSTZ

Latest

MSUVA HAKAMATIKIUNAKUMBUSHWA KUTUFOLLOW ILI UFAIDIKE NA OFA ZA EDUSPORTSTZ

Kiungo wa pembeni wa kimataifa, Simon Msuva, ameendeleza kufumania nyavu baada ya kuifungia timu yake ya Difaa Hassan El Jadida ya nchini Morocco.
Bao hilo alilifunga juzi Jumatano katika sare ya mabao 3-3 dhidi ya Chabab Atlas Khénifra katika mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco ‘Botola Pro’.

Katika mechi hiyo, Msuva aliyetua kuichezea timu hiyo mwanzoni mwa msimu huu akitokea Yanga, alifunga bao lake katika dakika ya 42.


Mabao mengine katika mchezo huo yalifungwa na Anouar Jayid dakika ya 82 na Adnane El Ouardy dakika ya 90.


Sare hiyo imefanya Difaa Hassan El Jadida kusogea hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi hiyo ikifikisha pointi 25.Wiki iliyopita, Msuva aliipigia hat-trick katika ushindi wa mabao 10-0 walioupata dhidi ya Benfica ya Guinea Bissau kwenye mechi ya raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Elimu Yetu
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz