KWA USHINDI HUU RUVU SHOOTING WATAJINASUA KUSHUKA DARAJA? - EDUSPORTSTZ

Latest

KWA USHINDI HUU RUVU SHOOTING WATAJINASUA KUSHUKA DARAJA?

Image result for RUVU SHOOTING

Ruvu Shooting imejinasua kutoka mkiani baada ya kuitwanga Kagera Sugar kwa mabao 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa kwenye Uwanja wa Mabatini, Pwani.



Ushindi huo umeifanya Ruvu Shooting kufikisha pointi 17 baada ya kuwa moja ya chini zilizo karibu na mkiani ikiwa na pointi 13.


Maafande hao walianza kupata bao lao la kwanza katika dakika ya 55 kupitia Hamis Mcha.


Wakati ikionekana kama wageni Kagera Sugar wangesawazisha, Shooting wakaongoza bao la pili kupitia Alinanuswe Martin katika dakika ya 79.


Kabla ya mechi hiyo, Msemaji wa Ruvu Shooting, alizungumza katika kipindi cha SPOTI HAUSI kinachorushwa na runinga ya mtandaoni ya Global TV na kusema timu yake itawashangaza wengi kwa kumaliza Ligi Kuu Bara katika nafasi ya tano.




“Tuna uhakika wa kubaki Ligi Kuu Bara tofauti na wengine wanavyofikiria, lakini nikuhakikishie hata nafasi ya tano tunaweza kushika.


“Ukiangalia kati yetu na aliye katika nafasi hiyo au hata kileleni, si pointi nyingi za kutisha, sisi tutamaliza tukiwa nafasi ya tano na inawezekana,” alisema Masau akionekana kujiamini.

NDG MSOMAJI WA EDUSPORTSTZ UNAKUMBUSHWA KUSUBSCRIBE NA KUFOLLOW WEB YETU PAMOJA NA MITANDAO YETU YA KIJAMII CHINI YA POSITI HII ILI KUTUMIWA UPDATES ZOTE ZA AJIRA, MICHEZO, HABARI, SCHOLARSHIPS PAMOJA NA MASTORI YA MASTAA NA VIONGOZI MBALIMBALI. EDUSPOTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO


EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz