TETESI ZA SOKA LA ULAYA JUMANNE YA LEO TAREHE 23.1.2018 - EDUSPORTSTZ

Latest

TETESI ZA SOKA LA ULAYA JUMANNE YA LEO TAREHE 23.1.2018




Mada zinazohusianaNDG MSOMAJI WA EDUSPORTSTZ UNAKUMBUSHWA KUSUBSCRIBE NA KUFOLLOW WEB YETU PAMOJA NA MITANDAO YETU YA KIJAMII CHINI YA POSITI HII ILI KUTUMIWA UPDATES ZOTE ZA AJIRA, MICHEZO, HABARI, SCHOLARSHIPS PAMOJA NA MASTORI YA MASTAA NA VIONGOZI MBALIMBALI. EDUSPOTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI.
Manchester City inamtaka Aymeric Laporte na inafikiria kutimiza kipengee cha kumruhusu beki wa kati huyo raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 23 kilichotolewa na Athletic Bilbao cha Pauni milioni 60. (Sun)

Borussia Dortmund inamtaka mshambuliaji raia wa Ufaransa wa timu ya Arsenal Olivier Giroud, mwenye umri wa miaka 31, kama sehemu ya kubadilishana na mchezaji raia wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, mwenye umri wa 28, - au wasitishe mpango huo hadi msimu wa joto. (Mirror)

Chelsea inatafakari kuvunja sera ya kutolipa malipo ya uhamisho kwa wachezaji wake kando na makipa walio na umri wa miaka 30, kumsajili mshambuliaji wa Bosnia Edin Dzeko, 31, kutoka Roma. Upande wa Antonio Conte huenda ukakamilisha makubaliano ya mara mbili ya Dzeko na mchezaji wa Roma Italia wa kiungo cha beki kushoto Emerson Palmieri, mwenye umri wa miaka 23, kwa thamani ya pauni milioni 44. (Telegraph)

Au Chelsea itawalipia wachezaji wote wawili pauni milioni 50. (Mirror)

Crystal Palace imeanzisha mazungumzo na Inter Milan kuhusu makubaliano ya zaidi ya pauni milioni 8.5 kumsajili mchezaji wa kiungo cha mbele Eder, mwenye umri wa 31. (Mail)

Newcastle ipo tayari kusaini uhamisho wa mkopo wa winga wa Chelsea raia wa Brazil Kenedy, mwenye umri wa miaka 21, katika saa 24 zijazo. (Mail)

Real Madrid inajitayarisha kwa uhamisho wakati wa msimu wa joto wa Mohamed Salah wa Liverpool mwenye umri wa miaka 25 kwa mujibu wa rais wa shirikisho la soka Misri. (Liverpool Echo)

Newcastle inashughulikia makubaliano ya kumleta mshambuliaji wa Atletico Madrid raia wa Ufaransa Kevin Gameiro, mwenye umri wa miaka 30, kuingia St James' Park. (Express)

Mshambuliaji wa West Ham Andy Carroll, mwenye umri wa miaka 29 yupo nje kwa miezi mitatu baada ya kufanyiwa upasuaji wa mguuu wake uliovunjika. (Telegraph)

Wasiwasi kuhusu afya ya Fabian Delph unamaanisha kuwa Manchester City inatazamia kumsaini mchezaji wa Shakhtar Donetsk kiungo cha kati mwenye umri wa miaka 24 Fred hivi sasa, badala ya kusubiri hadi msimu wa joto. (Manchester Evening News)

Winga wa Brazil Lucas Moura, 25, anayelengwa na Tottenham, anasema "hana raha" akiwa Paris St-Germain. (L'Equipe)

Meneja wa Bournemouth Eddie Howe anasema kurudi kwa winga Junior Stanislas, na mshambuliaji wa Norway Joshua King, mwenye umri wa miaka 26, kutoka kuuguza majeraha, ni kama kuwasajili wachezaji wawili. (Bournemouth Echo)


EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO

EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz